Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Mhe. Lameck Hole amewataka watumishi wote wa halmashauri kuongeza ushirikiano, uwajibikaji na kasi ya utendaji ili kuhakikisha utoaji wa huduma kwa wananchi unaboreshwa na miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi.
Akizungumza leo 18 Desemba 2025 katika kikao maalum kilichowakutanisha Mwenyekiti wa Halmashauri, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri pamoja na watumishi wa idara zote, Mwenyekiti amesema kuwa Halmashauri imeendelea kupiga hatua katika maeneo mbalimbali, lakini changamoto zilizopo zinahitaji nguvu ya pamoja kutoka kwa kila mtumishi
“Mafanikio ya Kwimba yanategemea uwajibikaji wa kila mmoja wenu, tunahitaji kufanya kazi kwa pamoja kwa uadilifu na kwa kasi inayokwenda sambamba na matarajio ya wananchi" amesema Hole
Pia amewataka watumishi kusimamia mipaka yao ya kazi na kuzitaka idara za mipango na manunuzi kuhakikisha wanapata taarifa kila siku kwenye maeneo yenye miradi.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya kwimba Dkt. Amon Mkoga amemhakikishia kumpa ushirikiano pia amewataka madiwani kutoa ushirikiano hasa katika suala la utekelezaji wa miradi kwa kushiriki usimamizi ili kuongeza ufanisi na kukamilisha miradi kwa wakati
“nikuhakikishie nitakupa ushirikiano pia niwaombe madiwani watusaidie kufuatilia taarifa za miradi na kusimamia miradi"
Aidha, Mkurugenzi amesisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya rasilimali, ufuatiliaji wa mara kwa mara wa miradi, na utoaji wa taarifa zinazoendana na matakwa ya kupanga maendeleo na kuhakikisha kuwa kila idara inakuwa sehemu ya suluhisho kwa changamoto za wananchi na si chanzo cha kukwamisha maendeleo .
“Tuanze ukurasa mpya wa ushirikiano na uwazi. Kwimba ina uwezo mkubwa wa kusonga mbele ikiwa tutadumisha mshikamano na kujituma katika majukumu yetu,” Mkoga
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.