Viongozi waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27,2024 wamepata mafunzo ya kuwaongoza katika kutekeleza majukumu yao.Mafunzo hayo yamefanyika katika tarafa tano za Halmashauri ya Kwimba ambapo wamesisitizwa uwajibikaji.
Katika mafunzo hayo mada mbalimbali zimewasilishwa ikiwa ni pamoja na majukumu ya Mwenyekiti wa Kijiji, Mwenyekiti wa kitongoji, majukumu ya mkutano mkuu wa kijiji na mambo mengine.
Aidha viongozi hao wamesisitizwa kutimiza wajibu wao ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye shughuli za maendeleo, kuhamasisha ulinzi na usalama, kuhamasisha mapato,kushiriki vikao vya kisheria na mikutano mingine.