Mkuu wa Wilaya ya Geita Mheshimiwa Hashimu Komba akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita amefungua maonesho ya saba ya Nanenane kanda ya ziwa magharibi huku akiwapongeza makatibu Tawala wa Mkoa ya Geita na Mwanza kwa kufanya maandalizi mazuri ya maonesho hayo.
" haya ni maonesho yanayozikutanisha sekta muhimu za kilimo,mifugo nauvuvi, wananchi wetu wengi wanategemea kilimo kwa hiyo maonesho haya yanawasaidia wananchi wetu kujifunza ukuaji wa teknolojia unavyoongeza tija kwenye kilimomo, mifugo na uvuvi"
Ametumia wasaa hu kuwasihi wananchi wote kutembelea mabanda ili wakapate elimu ya pembejeo bora, na elimu bora ya kilimo,mifugo,uvuvi na elimu ya kusindikika mazao.
Mkuu huyo ametumia kauli mbiu ya nanenane inayosema " chagua viongozi bora kwa maendeleo ya kilimo,mifugo na uvuvi" kuhamasisha wananchi kwenda kuchagua viongozi bora watakaoleta ubunifu na mabadiliko katika kilimo,mifugo na uvuvi"
Pia ametoa rai kwa mamlaka za Serikali za mitaa kutumia vyema mikopo ya asilimia kumi kwa vikundi vinavyojihusisha na sekta za kilimo,mifugo na uvuvi ili kuongeza ajira kwa vijana.
Akitoa taarifa ya maandalizi katibu Tawala msaidizi Mkoa wa Mwanza Peter amesema Wakulima na wananchi wanapata fulsa na kuona hudumaa zinazotolewa na wanajifunza jinsi teknolojia inavyoboresha sekta hizo.
Halmashauri 14 zinashiriki maonesho ya nanenane kanda ya ziwa maghalibi ambapo mwitikio wa wananchi ni mkubwa.
Naye mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Christopha Ngubiagai amesema " maazimisho ya nanenane yanaendelea kuwa jukwaa zuri kwa kuonesha ubunifi na teknolojia katika sekta ya kilimo
Maonesha haya yanaendelea kuwahamasisha wananchi kulima kisasa na kufuga ufugaji wenye tija, pia amehamasisha ubunifu katika shughuli za kilimo uongezeke zaidi ili wakulima waweze kunufaika zaidi.
Aidha amezipongeza taasisi zote zinazoshiriki maonesho hayo"ninazipongeza taasisi zote zinazoonesha mbegu mbalimbali zikiwemo mbegu za migomba"
Katika uzinduzi huo ameshiriki Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Kwimba Dkt Amon Mkoga ambaye anawakarisha wananchi kutembelea banda la Kwimba ili kujifunza kilimo na ufugaj