MARUKU KUWAWEKA WATOTO KWENYE MAGENGE YA BIASHARA NYAKATI ZA USIKU
Posted on: July 23rd, 2025
Haya nimaelekezo aliyoyatoa Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe Ng'wilabuzu Ludigija wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Runele
Mkutano huo umefanyika leo 23,Julai 2025 ambapo Mkuu wa Wilaya amehimiza wananchi kuhakikisha watoto wote wanapelekwa shuleni na siyo kuachwa nyumbani kwaajili ya kufanya biashara au kazi za nyumbani.
Pia ametoa onyo kwa wazazi wanaoozesha wanafunzi " usirihusu kukatisha masomo ya mtoto wako, na mzazi yoyote atakayeozesha mwananfunzi kama amelipwa ng'ombe tutazitaifisha zinakuwa mali ya Serikali na muoaji atafungwa miaka 30" Ludigija
Amesisitiza kuwa wako wanafunzi wanaacha shule kwa muda kidogo kisha wanaolewa, hao niwanafunzi wataacha kuwa mwanafunzi pale wanafunzi walioanza nao shule watakapohitimu.
Wananchi wa kijiji hicho wameiomba Serikali kusajili Shule shikizi iliyojengwa kitongoji cha Ibaya ili kuondoa usumbufu wanaoupata wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata shule.
Naye Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kwimba Deocres Mkandala ametoa elimu kwa Wananchi wa Runele kuhusu siku ya uchaguzi kuwa wanatakiwa kutunza vitambulisho vyao vya kupigia kura na hairuhusiwi kukusanya vitambulisho hivyo.
pia wameshauriwa baada ya kupiga kura watatakiwa kwenda nyumbani kusubiri matokeo siyo kukaa makundimakundi karibu na vituo vya kupigia kura, pia amewahamasisha kutoa taarifa kituo cha polisi pindi wanapopata taarifa za watu wanaofanya uhalifu wa aina yoyote