Waalimu, wahasibu na Waganga wafawidhi wa vituo vya Afya wapatiwa mafunzo ya Mfumo wa Serikali wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektronic "Government e-Payment Gateway System (GePG) Mfumo unaosimamiwa na Wizara ya Fedha na Miapngo.
Akitoa mafunzo hayo yaliyofanyika kuanzia tarehe 28, Machi hadi tarehe 6,Aprili 2022 muwezeahaji Bi. Magdalena Makombe amesema Mfumo huo ukitumika ipasavyo utasaidia kutatua changamoto zilizopo kwenye mfumo uliokuwepo hivyo uwazi na udhibiti wa fedha za umma utaongezeka.
Vilevile mfumo huu utasaidia kurahisisha namna ya kulipia huduma za Umma, kupunguza gharama zinazoambatana na ukusanyaji wa fedha za Umma, kutoa huduma bora na rahisi, itasaidia kupata taarifa sahihi kwa wakati sahihi na kupunguza gharama za uwekezajikatika miundombinu ya TEHAMA pamoha na " Software Development" katika suala la ukusanyaji wa mapato.
Nao walengwa wa mafunzo hayo wamesema kupitia Mfumo huo waliojifunza utawarahisishia kazi ya ukusanyaji wa mapato na utawaongezea ufanisi katika kazi zao.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.