Vijana waliohitimu mafunzo ya mgambo wameshauriwa kwenda kuhamasisha wananchi kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Haya yamesemwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba ndugu Mohamed Ngasinda wakati akifunga mafunzo ya mgambo yaliyokuwa yakifanyika Kata ya Bupamwa
" mmeonyesha hali ya ukakamavu na uzalendo mliojifunza kupitia mafunzo haya, nendeni mkawahamasishe wananchi kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa, kwani kuwa na Taifa salama ni pamoja na kupata viongozi bora katika maeneo yetu" amesema Mohamed
Aidha Katibu Tawala amewataka vijana hao kuwa wazalendo kama walivyofundishwa na wametakiwa kushirikiana na jamii kuimarisha ulinzi na usalama katika vijiji vyao.
Akiwasilisha taarifa ya mafunzo hayo Mshauri wa mgambo Stanley Wambura amesema vijana hao wamepata mafunzo mbalimbali yakiwemo mafunzo ya ukakamavu, matumizi ya siraha ndogondogo, utunzaji wa mazingira, athari na matumizi ya vyombo vya habari, mbinu za kivita na uokoaji.
Wahitimu hao wakisoma risala yao wameeleza changamoto mbalimbali ambazo Katibu Tawala ameahidi kuzishugulikia na kuzitatua.
Vijana waliohitimu mafunzo hayo ni 42 wakike 13 na wakiume 29 kati ya 44 walioanza mafunzo hayo ambapo vijana wawili waliahirisha mafunzo na kwenda masomoni.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.