• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

Mhe. Jaffo apongeza ujenzi wa kituo cha kutolea huduma za Afya Malya

Posted on: July 5th, 2018


Mhe.Selemani Jaffo (MB), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI)  ametoa pongezi zake kwa uongozi wa Halmashauiri ya Wilaya ya Kwimba kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa jengo la Upasuaji, Wodi ya akinamama, Maabara, Chumba cha kuhifadhia maiti na Nyumba moja ya mtumishi katika ujenzi wa kituo hicho.

“Kituo hiki cha kutolea huduma Malya kwa moyo wangu wa dhati  mmekitendea haki sana”

Hayo aliyasema Mhe. Jaffo wakati wa ziara ya kutembelea kituo hicho tarehe 05 /07/ 2018 Wilayani Kwimba.



      Mhe.Selemani Jaffo  akiongea na wananchi wa kata ya Malya.

Mhe. Jaffo alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  DKT. John Pombe Magufuli kwa moyo alionao wa kuwatumikia watanzani katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya afya.

“Mhe Rais hatawaangusha katika kipindi chake cha uongozi, anahakikisha fedha zote zinazowahusu watanzania zinawafikia pamoja na miradi iliyosimama kwa mda mrefu inakamilika,”

Pamoja na kumpongeza Rais, Mhe. Jaffo amewataka wananchi wa kata ya malya kuhakikisha wanajiunga na Mfuko wa Jamii (CHF) iliyoboreshwa kwa ajili ya  kupunguza gharama za matibabu.

Aidha Mhe. Jaffo amemtaka Mganga Mkuu wa Wilaya Dr.Elias Misana kuhakikisha kituo cha afya Malya kinafungwa mfumo wa utoaji taarifa za  ukusanyaji wa mapato ya hospitali (GHOMIS).

Mhe.Selemani Jaffo  akiweka jiwe la msingi katika mradi wa Ujenzi wa kituo cha kutolea huduma za afya Malya.

Kwa kuongezea Mhe. Jaffo amemuagiza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) Dr. Zainabu Chaula  kuhakikisha anatenga fedha maalum kwa ajili ya ujenzi wa jengo maalum la “Utrasound”  na  “Exray” Mashine  kwa lengo la kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Naye Mbunge wa Jimbo la Sumve Mhe. Richard Ndassa amezishukuru kamati zote kwa moyo  wa kujitolea usiku na mchana ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa kiwango kilichokusudiwa pamoja na kufuata maagizo waliokuwa wanapewa na wataalam kutoka Wilayani.

Kwa upande wake Mkuu wa  Wilaya ya Kwimba Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon amesema changamoto kubwa inayovikumba vituo vya kutolea huduma ni pamoja  na upungufu wa watumishi hivyo basi amemuomba Mhe. Jaffo kuhakikisha  kituo cha afya Malya kinapata watumishi wa kutosha ili  kiweze kufanya kazi iliyodhamiliwa na hatimaye wananchi waweze kufurahia maendeleo ya nchi yao.

Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ilipokea jumla ya shillingi millioni 400,000,000/= kwa ajili ya ujenzi i wa kituo hicho kwa lengo la kutekeleza mkakati wa serikali wa kuviboresha na kujenga vituo vya kutolea huduma za afya nchini ili viweze kutoa huduma bora inayoendana na mahitaji halisi ya wananchi.

 

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.