"tunapokuwa tunaadhimisha miaka 63 ya Uhuru tunajivunia amani na maendeleo ambayo Baba wa Taifa alianzisha na viongozi waliofuata wanaendeleza, pia tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za maendelo barabara,elimu ,afya na miradi mingine"
Kauli hii imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija wakati wa mdahalo uliokuwa ukijadili maendeleo katika sekta mbalimbali hapa Wilayani Kwimba baada ya Uhuru wa Tanganyika
" Serikali imefanya kazi kubwa sana na hapa Kwimba tumepiga hatua kubwa kwa mfano barabara kutoka hapa ngudu kwenda Mwanza mjini tulisafiri zaidi ya masaa sita lakini kwa sasa barabara zimeboreshwa sana tunatumia saa moja na nusu" Ludigija
Mkuu wa Wilaya amesisitiza kuwa Wilaya ya Kwimba kabla ya Uhuru kulikuwa na Shule tano tu lakini kwa sasa kuna shule zaidi ya 200 za msingi na Sekondari hivyo maendeleo ni makubwa.
Akielezea kauli mbiu ya miaka 63 ya Uhuru inayosema "JITOKEZE KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 KWA AMANI NA UTULIVU" Pia ametumia wasaa huo kuwaasa wananchi kuwa tayari kushiriki uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2025, ambapo amesisitiza amani na usalama katika kipindi chote.
Nao wazee maarufu waliokuwepo enzo za Uhuru ambao wameshiriki mdahalo wameelezea jinsi Kwimba ilivyo na maendeleo makubwa kwani miaka 63 iliyopita hakukuwa na barabara za lami, hakukuwa na maji kila mahali, vituo vya afya vilikuwa vichache hata umeme haukuwepo walitumia vibatari, lakini kwa sasa vitu vyote vipo japo bado kuna changamoto chache.
Katika mdahalo huo wanafunzi kutoka Shule za sekondali wametoa hoja mbalimbali zikionyesha jinsi Taifa lilivyopiga hatua kwenye miundombinu ya barabara, Elimu, maji Afya na Umeme na miradi mingine.
Aidha watu wenye mahitaji maalumu wameshiriki mdahalo huo ambapo nao wameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwajali hasa kwa kuwapatia mikopo kwaajili ya vikundi vya ujasiliamari.