MILIONI 700 ZINATARAJIWA KUTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU
Posted on: January 21st, 2025
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba inaendelea kutoa mafunzo kwa vikundi vilivyoomba mikopo isiyo na riba ya fedha zinazotokana na asilimia kumi ya mapato ya ndani, leo Januari 21,2025 mafunzo ya namna bora ya kwenda kutumia fedha hizo yametolewa kwa vikundi 37 vinavyotarajia kukopeshwa milioni 607.
Akifungua mafunzo hayo Katibu Tawala wa Wilaya ndugu Mohamed Ngasinda amewataka wajasiliamali hao kwenda kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa
" mimi niwapongeze kwasababu mmejidhatiti kwenda kutumia huu mkopo maana tumekagua kazi zunu mnajitahidi, sasa niwasisitize kwenda kutimiza lengo la fedha hizi, hizi fedha siyo msaada, hii nimikopo haina riba kwahiyo kazi yako ni kwenda kuzarisha na kurejesha ili na wengine wakopeshwe" Ngasinda
Akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa shughuli hiyo Afisa maendeleo wa Wilaya Bi. Rozalia Magoti amewataka wote watakaokopeshwa kuwa waaminifu katika kurejesha fedha hizo
" hatutegemei vikundi hivi kukamatwa na polisi kwasababu ya kushindwa kurejesha, mafunzo tumewapa kafanyeni kazi, zarisheni na mrejeshe kwa wakati" Magoti
Katika mafunzo hayo ameshiriki Kamanda wa TAKUKURU Kwimba ndugu Juliani Agustine ambaye amevitaka vikundi vyote kutoa taarifa pindi watakapoombwa rushwa na mtu yeyote.
Naye muwakilishi wa jeshi la Polisi Kamanda Deocres Mkandala amewashauri kuzingatia maandiko yao ya biashara ili kwenda kutumia fedha kwa lengo lililokusudiwa, na kurejesha fedha hizo kwa wakati ili kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza.
Vikundi 37 kati ya 70 vimekidhi vigezo vya kupewa mikopo hiyo huku vikundi vilivyosalia vikishauriwa kwenda kuboresha taarifa zao na kuweka sawa miradi yao ili vikopeshwe awamu itakayofuata.