• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

Mkoa wa Mwanza Watosha kuandaa Maadhimisho ya Nanenane Kitaifa

Posted on: August 5th, 2017

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongera amesema mpaka sasa Mwanza inatosha kuandaa maonyesho ya Sherehe za nanenane Kitaifa  amemuomba  Mwakilishi wa Katibu Mkuu kutumia vigezo vyao ili maonyesho ya nanenane kitaifa  kwa mwaka 2018 yafanyike katika Mkoa wa Mwanza.

“Mtupe maelekezo ya kufanya na sasa kanda ya ziwa inasubiri na zamu yetu imefika kuandaa maonesho ya sherehe za nanenane Kitaifa.”

Ameyasema hayo wakati akifungua Rasmi Maonyesho ya Sherehe za Wakulima   tarehe  o4 Agost,2017  katika uwanja wa Nyamhongoro Mkoani Mwanza.

Aidha amesema kuanzia sasa kanda ya ziwa inajipanga kutatua changamoto za miundombinu katika uwanja wa Nyamhongolo.

“ kuelekea maadhimisho ya mwaka 2018 tunaanza mara moja ujenzi wa miundombinu ya kudumu tunapokuja kwenye maonyesho haya mwaka kesho tutakuta uwanja unakiwango kikubwa cha ujenzi  na uwekezaji wa miundombinu ya kudumu nayakisasa kwa kushirikiana na wakuu wa mikoa na wakurugenzi wote wa kanda ya ziwa.”

Mhe. Mongera ameendelea kumpongeza na kumshukuru Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  kwa kuweka  msisitizo mkubwa kwenye viwanda.Amesema  kuwa dhana hii ya viwanda haiwezi kukamilika bila ya kuwa na mabadiliko makubwa kwenye sekta ya kilimo na asilimia themanini ya wananchi wanajishughulisha na shughuli za uzalishaji mali kupitia  kilimo cha mazao, ufugaji na uvuvi hivyo wataamu waendelee kuwaamasisha wananchi kujishughulusha na shughuli za kilimo bora ili kufikia uchumi wa kati.

Naye kaimu mkuu wa Wilaya ya Ilemera Mhe. Khadija Nyembo ameishukuru kamati ya Maandalizi ya Sherehe za nanenane kwa kuandaa maonyesho hayo mazuri.Mhe.Nyembo ameyasema hayo wakati akimkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kuongea na wakulima wa kanda ya ziwa.

Pia Ndg Mathayo Mabirika  mjasiliamali kutoka katika kikundi cha Mahiga wilayani Kwimba amesema maonyesho ya mwaka huu  ni ya kipekee kwani idadi ya washiriki wa sherehe za maonyesho ya nanenane na wananchi wanaokuja kwa ajilili ya kununua bidhaa za wakulima ni wengi  ukitofautisha na sherehe za mwaka jana 2016.



Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bibi Pendo A.Malabeja akisalimiana na Mkulima wa Zao la Mpunga Ndg Mathayo Mabirika katika Banda la Maonyesho ya Kilimo la Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

Maonyesho ya  ya sherehe za wakulima nanenane ni ya tano (05)  kwa mikoa ya kanda ya ziwa ikiwemo Mara,Simiyu Geita, Mwanza,Kagera na Shinyanga  kufanyika katika viwanja vya Nyamhongoro Mkoani Mwanza.Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati ya  Maandalizi  ya Shrerehe za  Wakulima Nanenane Ndg.Beda Chematata.

  

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.