Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Dkt. Amon Mkoga ametoa siku tano kwa wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa madarasa Mwanekeyi kuhakikisha ujenzi huo unaanza kutekelezwa mara moja
"nawapa siku tano kuhakikisha miradi yote ujenzi wake unafanyika kuanzia sasa, baada ya siku tano nitarudi hapa Mwanekeyi kukagua mradi huu “ amesema Mkoga
Ameyasema hayo Novemba 12, 2025 wakati akifanya ziara ya Kata kwa Kata kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Kata zote za Kwimba ikiwemo ujenzi wa Shule mpya za Msingi na Sekondari na ujenzi wa vituo vya Afya na Zahanati.
Pia amewataka wasimamimizi wa miradi ngazi ya Kata kuwafichua watu wanaokwamisha utekelezaji wa miradi hiyo ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria
Aidha amewapongeza wasimamizi wa miradi ya ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari walla iliyopo Kata ya Walla na shule ya msingi chamva iliyopo kata ya Nkalalo na kuwataka kuongeza juhudi zaidi ili kukamilisha miradi kwa wakati.
Vilevile ametumia ziara hiyo kuongea na watumishi wa Kata ya Walla na Nkalalo ambapo amewasisitiza kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanatimiza wajibu wao.

Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.