MKULIMA KUTOKA KWIMBA AIBUKA MSHINDI WA KWANZA ZAO LA PAMBALA PAMBA
Posted on: August 8th, 2025
Katika kuhitimisha sherehe za wakulima nanenane wakulima wa mazao mbalimbali wameshindanishwa kutokana na vigezovilivyowekwa na kamati ya maandalizi ya ya sherehe ambapo Mkulima kutoka Kwimba Ndugu Ngulimi John Zakalia amekuwa mshindi wa kwanza katika kipengele cha mkulima bora wa zao la Pamba
Akiwasilisha taarifa ya maonesho ya nanenane Mkuu wa sekisheni ya uchumi Mkoa wa Mwanza Ndugu Peter Masele amesema haya ni maonesho ya saba ya kanda ya ziwa magharibi ambapo wadau mbalimbali wameshiriki maonesho hayo zikiwemo taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi, pamoja na wajasiliamali, "tunaamini kuwa maonesho haya washiriki watayatumia vyema kuongeza tija katika shughuli za kilimo,mifugo na uvuvi"
Mheshimiwa Martin Shigela Mkuu wa Mkoa wa Geita akimkaribisha mgeni rasmi wa sherehe hizo amesema maonesho yamefana sana kuliko mwaka jana pia amewashukuru wananchi kwa kushiriki maonesho hayo.
Aidha amemshukuru Rais kwa kuwezesha wananchi kupata pembejeo na vifaa vingine vya kilimo ikiwemo mbolea ya ruzuku ambayo imechangia kuongeza uzalishaji kwa wakulima.
Mgeni rasmi wa sherehe hiyo Mheshimiwa Saidi Mtanda Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akihitimisha maonesho hayo amesema
" nimefanikiwa kupita kwenye mabanda nimeona na kujifunza teknolojia mbalimbali, hata mimi ni mkulima na nimenufaika na maonesho haya, twende tukatumie elimu tuliyoipata hapa kuboresha uzalishaji katika kilimo,mifugo na uvuvi"
Pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwaajili ya chanjo ya kuku na chanjo ya mifugo mingine.
Amesisitiza kuwa sekta ya kilimo ndio imeajili watu wengi hivyo ni eneo nyeti ndiyo maana Serikali imewekaza katika sekata hii ili kuboresha uchumi wa watu wengi
Pia ametumia kauli mbiu ya maonesho hayo inayosema " chagua kiongozi bora kwa maendeleo ya kilimo,mifugo na uvuvi" kuwahamasisha wananchi wote kujitokeza kupiga kura ifikapo Oktoba 2025 ili kuchagua viongozi bora watakaohamasisha maendeleo ya kilimo mifugo na uvuvi.