MKURUGENZI ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI KATIKA HOSPITALI YA WILAYA
Posted on: February 20th, 2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Dkt Amon Mkoga amesikiliza kero za wananchi na wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ambapo kero na changamoto zilizowasilishwa zimetatuliwa
" kila jumatano ni siku ya kusikiliza kero za wananchi na hapa hospitali ndilo eneo litakalotumika kusikiliza kero hizo kwahiyo watu wote wenye changamoto ziwasilisheni hapa ili tuzipatie ufumbuzi" amesema Mkoga
Wananchi walioshiriki kikao hicho wamewasilisha kero zao, ikiwemo kero ya upatikanaji wa dawa, usumbufu wa mfumo na kucheleweshwa kwa baadhi ya huduma hapo hospitali
" changamoto ya upatikanaji wa dawa itatuliwe sitaki kusikia hakuna dawa yaani dawa ikikosekana hapa basi wilaya nzima hiyo dawa isiwepi" amesema Mkurugenzi akimuelekeza Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo.
Aidha Mkoga amewataka watumishi wa Idara ya afya kuhakikisha wanaboresha huduma na kufanya kazi kwa weledi huku wakizingatia taratibu, sheria na kanuni zinazoongoza watumishi wa umma
" mpe mtu mawasiliano ya kuridhisha wagonjwa ndio wateja wenu siyo mtu anakuja Maabara unamwambia jina halipo badara yake muelekeze vizuri kwamba jina lako halijatumwa rudi kwa daktari atume tena, tumieni kauli nzuri" amesema Mkoga
Mkurugenzi huyo ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wenye changamoto na kero kufika kila siku ya jumatano katika ukumbi wa hospitali ya Wilaya ( Icheja) hapo kero zitasikilizwa na kutatuliwa.