Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Dkt.Amon Mkoga amewataka wasimamizi wa miradi ya maendeleo kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa weledi.
Haya yamejiri jana Novemba 2,2024 wakati akikagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa jimbo la Kwimba
" kila mtu atimize wajibu wake staki kusikia eti mradi umekwa wakati Serikali imetoa fedha, anayekwamisha mradi nitamchukulia hatua kali" amesema Mkoga
Katika ziara hiyo miradi mbalimbali imekaguliwa ikiwa ni pamoja na miradi ya elimu,Afya na utawala ambapo kasi ya utekelezaji wa miradi imetakiwa kuongezwa ili miradi yote ikamilike kwa wakati.
Miradi ya elimu iliyokaguliwa ni ujenzi wa mabweni shule ya sekondari Nyamilama, ujenzi wa shule ya msingi shikizi Nyanhiga, ujenzi wa madarasa shule ya msingi Ilula, ujenzi wa madarasa matatu shule ya msingi Shigangama,ujenzi wa choo shule ya sekondari Shilembo, ukamilishaji wa darasa shule ya msingi Kawekamo,ukamilishaji wa darasa shule ya Sekondari Mwamashimba, ujenzi wa madarasa matatu shule ya msingi Mwang'anga, ujenzi wa vyoo shule ya msingi Mwamitinje, ujenzi wa madarasa shule ya msingi Chasalawi na Kiliwi, ujenzi wa madarasa shule ya Msingi Buyogo, Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Kabale Ng'undi na ujenzi wa shule mpya ya msingi ya mchepuo wa kiingeleza Icheja.
Miradi ya Afya iliyokaguliwa ni ujenzi wa tenkila maji na choo zahanati ya Kibitilwa, ukamilishaji wa zahanati ya Manguluma,ukamilishaji wa jengo la kusubiria wagonjwa katika hospitali ya Wilaya( icheja) na mradi wa utawala uliokaguliwa ni jengo la utawala la Halmashauri linalojengwa icheja Ngudu.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.