• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

MKURUGENZI AWATAKA WALIMU WAKUU KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA UFASAHA

Posted on: October 8th, 2021

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba awataka Wakuu wa Shule na Walimu wakuu kufanya kazi kwa upendo, ushirikiano na uadilifu. Ameyasema haya kwenye kikao cha robo cha Tathmini ya Shughuli za Elimu, ambacho kimefanyika leo tarehe 08, Oktoba 2021 kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ngudu.


Mkurugenzi huyo amewataka Walimu kufanya kazi kulingana na sheria na taratibu za utumishi.


Amewasisitiza Walimu kusimamia miradi inayotekelezwa katika Shule zao kwa uadilifu. Aidha amesema Walimu wanapaswa  kuzingatia miongozo katika utoaji wa adhabu kwa Wanafunzi. "Narudia tena tuache kutoa adhabu zisizo na Afya kwa Wanafunzi" amesema Bi. Happiness Msanga


Mkurugenzi huyo amewataka Walimu kuacha ulevi na amewataka walimu wakuu kutoa taarifa za Walimu walevi ili wachukuliwe hatua, amesisitiza kuwa haizuiliwi kunywa pombe lakini pombe hairuhusiwi  mda wa kazi kwa watumishi


"wape masikini kilevi wasahau shida zao lakini kilevi hakifai kwa Mfalme asije potosha hukumu" amesema Msanga


Bi. Msanga amewashauri Walimu hao kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii katika maeneo yao wanayoishi.


Katika kikao hicho ameshiriki Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza  Mwalimu Martine Nkwabi ambaye amewataka Walimu kufanya kwazi kwa kuzingatia miongozo, aidha amesisitiza uadilifu katika kusimamia miradi inayotekelezwa na amewataka Walimu wanaopewa nafasi za kuwasimamia wengine kuzitendee haki nafasi hizo.


Amewataka walimu wanaojihusisha na mahusiano ya kimapenzi na Wanafunzi kuacha mara moja tabia hiyo, " ninachokiona tutapata upungufu wa Walimu kwa sababu wengi watafungwa" amesema Nkwabi



Afisa Elimu huyo amesisitiza kuwa heshima ya mtumishi hailetwi na mavazi, vyeti vyenye A nyingi, utanashati au mali ila heshima inaletwa na huduma anayotoa katika jamii.

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.