Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Dkt.Amon Mkoga amewataka watumishi wote kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma huku akisisitiza upendo na uadilifu miongoni mwa watumishi
" fanyeni kazi kwa upendo, uadilifu na mheshimiane, watumishi wote muwaheshimu wakuu wenu wa Idara na vitengo" amesema Mkoga
Mkuu huyo amewasisitiza watumishi wote kuwa na siha njema wanapokuwa kazini huku akikazia haiba katika mavazi na mazungumzo " watumishi wote mnatakiwa kuvaa vizuri mavazi yenu ya mitaani msiyalete hapa kazini, hapa kila mtu avae kulingana na taratibu za uvaaji kwa watumishi "
Aidha Mkuu huyo amewataka wakuu wa Idara na vitengo kuwachukulia hatua watumishi wote wasiofata sheria,taratibu na kanuni za utumishi wa umma.
Katika kikao hicho ameshiriki Afisa uchaguzi Ndug. Wiliam Kasuja ambaye ametumia nafasi hiyo kuwatangazia watumishi kujitokeza kwenye uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura awamu ya pili ambapo kazi hiyo inatarajiwa kuanza tarehe 1-7, Mei 2025 ambapo vituo vitavyotumika ni vilevile vilivyotumika awamu iliyopita
Watumishi walioshiriki kikao hicho wameahidi kwenda kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.