• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Afanya Ziara ya Kutembelea Miradi ya Maendeleo

Posted on: September 18th, 2017

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, Bibi Pendo A. Malabeja  amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kutumia Fedha za Ruzuku ya Maendeleo (CDG), Malipo kwa ufanisi (P4R na RBF)) katika maeneo mbalimbali ambayo miradi hiyo inatekelezwa.

Katika ziara yake, Mkurugenzi Mtendaji, aliweza kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa katika shule ya msingi Kiliwi,  Shule ya Sekondari  Bupamwa, Kituo cha Afya Mwamashimba, Shule ya Sekondari Mwamashimba, Shule ya Sekondari Talo, Zahanati ya Manawa,  Kituo cha Afya Malya na Eneo la Maegesho ya Magari Hungumalwa.

Akiwa katika ziara hiyo,Bibi Pendo A. Malabeja alisisitiza na kuwaelekeza wasimamizi wa miradi kuwa Fedha za miradi ya maendeleo zilizopatikana zitumike katika miradi ambayo ni kipaumbele ili iweze kutatua changamoto zinazowakabili wananchi. Aliyasema hayo wakati wa kikao kifupi kilichofanyika katika shule ya Sekondari Mwamashimba

Aidha Bibi Pendo  alimuagiza kaimu Mhandisi wa Ujenzi Ndugu Edwin Machumu kuhakiksha michoro ya  mabweni ya shule ya sekondari mwamashimba inapatikana haraka iwezekanavyo ili mradi huo uweze kuanza na kumalizika kwa wakati.

Naye Afisa Elimu Sekondari Ndg Lawi Kajanja aliwaagiza Wakuu wa shule kuhakikisha wanatunza kumbukumbu za miradi kwa kufungua jalada la kila mradi.

Sanjari na maelekezo ya Mkurugenzi Mtendaji, Mkaguzi wa Ndani Ndg Maro Kenyuko aliwataka Watendaji Kata na Vijiji kuhakisha wanasoma  taarifa za  mapato na matumizi kwenye mikutano na vikao vya ngazi ya chini ili kuondokana na migogoro isiyo na msingi na kuhakikisha kila mmoja ana daftari la kumbukumbu/maelekezo.

Bibi Pendo A. Malabeja aliupongeza uongozi wa Zahanati ya Mwamashimba chini ya usimamizi wa Dkt. Paul Swakala  kwa namna walivyosimamia vizuri ukamilishaji wa jengo la upasuaji ambalo litapunguza vifo vya mama na mtoto chini ya miaka mitano vinavyotokana na uzazi.

Mkurugenzi mtendaji, alihitimisha ziara yake kwa kuendelea kuwasisitiza Wakuu wa shule na waganga wakuu  wa vituo vya afya kuhakikisha fedha za miradi zinatumika kama zilivyopangwa na miradi inakamilika kwa wakati bila kuwa na kisingizio chochote.

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.