• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Afungua Mafunzo ya Mfumo wa FFARS

Posted on: June 13th, 2017

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bibi Pendo A. Malabeja  amefungua mafunzo ya  mfumo wa Uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma   ujulikanao kwa Kiingereza kama Facility Financing Accounting and Reporting System (FFARS) kwa Mhasibu wa Hospital ya Wilaya, Wakuu  wa Vituo vya Afya na Waratibu Elimu Kata yaliyotolewa na OR-TAMISEMI kwa kushirikiana na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma yaani Public Sector System Strengthening   (PS3) katika Ukumbi wa Chama cha Walimu (CWT) Kwimba tarehe 12/06/2017.

Akifungua mafunzo hayo; Bibi Pendo A. Malabeja amewaomba washiriki wa Mafunzo  kuzingatia  mafunzo hayo kwa umakini wa hali ya juu kwani  watakwenda kufundisha watumishi wa Mamlaka za Serikari za Mitaa kwenye vituo vya kutolea  huduma (Zahanati,Shule za Msingi na Sekondari)

Kwa upande wake mshauri wa masuala ya fedha (PS3) Bwana Martin Lawi amewataka washiriki wa mafunzo wawe kitovu cha mabadiliko kwa ajili ya mifumo na kuhakikisha taarifa za fedha zinaandaliwa kwa usahihi na zinatumwa kwa wakati makao makuu ya wilaya kila mwezi na kila robo ya mwaka.

Aidha mshiriki wa Mafunzo Bwana Jackson John Stephano ambaye ni Mratibu Elimu Kata ya Ngudu amesema mafunzo yamewajengea uwezo wa kutosha kwa upande wa “manual”  hivyo basi wanahitaji mafunzo mengine kwa upande wa Kielektroniki kwa ajili ya ufanisi zaidi.





Washiriki wa Mafunzo ya mfumo wa Uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma wakisikiliza kwa makini  Mada zinazofundishwa na wakufunzi.


Kwa kuhitimisha mafunzo hayo Mratibu wa PS3 Halmashauri ya wilaya ya kwimba Bwana Yohana Mhandikila ametoa shukrani zake kwa  watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), pamoja na Mradi wa PS3, na wadau wote waliohakikisha mfumo huu unakuwepo, ambao ni: Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Wizara ya Fedha na Mipango; Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi; na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Halmashauri ya wilaya ya Kwimba ina jumla ya vituo vya afya vitano (05), Zahanati Aarobaini na nne (44) ,Hospitali moja (01), Shule za msingi  mia moja hamsini na moja (151) na Sekondari  thelathini na tano (35)  Mafunzo haya yatasaidia kuhakikisha watoa huduma katika vituo wanapata ujuzi wa kutosha katika usimamizi wa fedha na kutoa huduma bora kwa wananchi wote na jamii zenye uhitaji.

Imetolewa na:

Kitengo cha Habari na uhusiano

Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.

13/06/2017

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.