Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Kigoma Malima amefanya ziara Wilayani Kwimba leo tarehe 5,Agosti 2022. Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa amejitambulisha na kutoa maelekezo kwa viongozi wa Wilaya na Halmashauri
“Kwenye uongozi wangu sitaki miradi ichelewe kukamilika, miradi ya maji ikamilike kwa wakati maana ikichelewa kukamilika anayelaumiwa ni Rais siyo watendaji. Tengenezeni mikakati itakayowawezesha watu wa Kwimba kupata maji”
Aidha amesisitiza asilimia kumi ya vijana,wanawake na Watu wenye ulemavu itolewe kama ilivyokusudiwa kutokana na mapato ya Halmashauri.
Mkuu huyo Amemtaka mganga Mkuu wa Wilaya kufanya tathimini ili kuhakikisha Hospitali ya Wilaya inaanza kutoa huduma zote zinazopatikana kwenye hospitali ya Wilaya,” naomba muangalie uwezekano wa kupeleka huduma zote za Afya huko kwenye Hospitali ya Wilaya”
Aidha Mheshimiwa Malima amempongeza Afisa Kilimo wa Wilaya ya Kwimba Mhandisi Magreth Kavalo kwa kusimamia uzalishaji wa mazao hasa ya Pamba na mazao mengine, pia amemuelekeza Afisa huyo kutengeneza mikakati itakayoongeza tija kwa Mkulima wa Pamba,dengu na mazao mengine
“ kazi kubwa inayofanyika Kwimba ni kilimo kwahiyo nikuelekeze kuweka mikakati itakayoongeza tija kwenye kilimo”
Ameshauli zao la mkonge lihamasishwe kwa Wananchi ili waone umuhimu wa kulima zao hilo kwani linafaida kubwa likianza kuvunwa ni miaka 12 mfululizo mkulima atavuna, pia ameahidi kusaidia upatikanaji wa mbegu za mkonge ili zitumike kulima shamba la mfano.
Akihitimisha kikao hicho amewaelekeza viongozi wote kufanya kazi kwa upendo,ushirikiano na umoja ili kuhakikisha malengo ya kutoa huduma kwa wananchi yanatekelezwa.
Katika ziara hiyo ameshiriki Katibu tawala Ndugu Baranja Mayuganya Elikana ambaye amewataka viongozi kufanya kazi ili kutimiza malengo ya Serikali
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Johari Mussa Samizi akisoma taarifa amesema Wilaya ya Kwimba inaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo miradi ya kilimo,Elimu,Afya,maji,Umeme,Barabara na miradi mingine.Aidha amesisitiza kuwa maandalizi ya Sensa yanaendelea na elimu inaendelea kutolewa kwa wananchi.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.