• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

MKUU WA MKOA WA MWANZA AFUNGUA MAONYESHO YA NANENANE

Posted on: August 4th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Kigoma Malima  afungua maonyesho ya nanenane kwa kuwataka wakulima kutumia kanuni bora za uzalishaji ili kufikia mwaka 2030  Tanzania tuwe tumefikia asilimia 10 za uzalishaji kwenye pato la Taifa.


Ufunguzi huo umefanyika leo tarehe 4,Agosti 2022 katika viwanja vya Nyamhongolo Mwanza. Akifanya ufunguzi huo Mkuu wa Mkoa amewasisitiza Wananchi kutumia fulsa za uwepo wa ziwa na mashamba kwaajili ya kuendeleza kilimo na ufugaji wa kisasa

“ Mkoa wa Mwanza unaeneo kubwa linalowezesha shughuli za uvuvi hasa kwa kutumia  vizimba, niwashauri mtumie ziwa kufuga kisasa ili kupitia ufugaji huo uchumi wetu uongezeke zaidi” Aidha amesisitiza Elimu kuhusu ufagaji wa kisasa itolewe kwa vikundi vya vijana ili iwasaidie kujiendeleza kiuchumi.


Aidha Mkuu wa Mkoa ameshauri taasisi za fedha zitumike ili kupata mikopo ya kuendeleza shughuli za kilimo ili zisaidie kuimalisha usalama wa chakula na kuongeza kipato kwa wakulima na wafugaji.

Mkuu huyo amesema Lengo la Mheshimiwa Rais  Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha viwanda vinavyotumia bidhaa za kilimo vinaongezeka zaidi ili mazao yanayozalishwa yaongezewe dhamani na ajira kwa vijana ziongezeke.


Maonyesho ya nanenane  yamelenga  kuwaonyesha wakulima na wadau wengine kuwa kilimo kinaweza kumfikisha mkulima mahali anapotaka kufika kama ataamua kulima na kufuga  kisasa.


Mheshimiwa Malima ameitumia nafasi hiyo kutoa  elimu ya sensa kwa wananchi huku akisisitiza umuhimu wa takwimu za idadi ya watu na makazi ili kuirahisishia Serikali kupanga mikakati ya maendeleo

” niwaombeni wote mjipange kushirki siku ya Sensa, wote tutoe ushirikiano kwa wakusanya takwimu”


Akikagua mabanda ya maonyesho amepita banda la Kwimba ambapo amesisitiza elimu ya kilimo cha  Maboga makubwa, Pamba, dengu na mazao mengine  itolewe kwa Wananchi ili kilimo hicho kilete tija kwa Wananchi.

“ nitamfatilia huyu mama anayelenga kupanda hizi mbegu za Boga ili nione kama atapata maboga makubwa kama haya mnayotuonyesha watu wa Kwimba, toeni elimu na wasaidieni  wakulima wanaolenga kufanya kilimo cha mazao yanayopatikana Kwimba” amesema Adam Malima

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.