• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

MKUU WA WILAYA AZINDUA OPERESHENI YA ANWANI ZA MAKAZI

Posted on: February 16th, 2022

Mheshimiwa Johari Mussa Samizi  amefanya uzinduzi wa anwani za makazi kwa kubandika namba kwenye Nyumba na kuweka bango la kuonyesha jina la Mtaa au barabara. Zoezi hili limefanyika leo tarehe 16 Feb, 2022 katika barabara ya Klasta na Fimbo.


Aidha Mheshimiwa Samizi amewaomba Wananchi wa Wilaya ya Kwimba kujitokeza kupendekeza majina ya Mtaa wanayoyapenda na kujitolea kutengeneza vibao vya majina hayo ili kila mtu ashiriki katika kazi hiyo.


Mkuu huyo amesisitiza kuwa uwekaji wa anwani hizi za makazi ni muhimu kwani zitasaidia kurahisisha  kufahamika kwa maeneo vilevile zitapunguza usumbufu uliokuwa unajitokeza pale mtu anapokuwa akielekea sehemu asiyoifahamu, kwani anwani hizi zikiishaingizwa kwenye mtandao zitamrahisishia mtu kutafuta mahali anapotaka kwenda kwa kutumia mtandao. Pia amesisitiza kuwa kukamilika kwa anwani hizi kutasaidia kurahisisha shughuli za Sensa.


" tengenezeni vibao vya majina yenu lakini yawe majina mazuri kwamaana ya majina yenye maana nzuri na yanayotambulika na kueleweka" amesema Samizi


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amewapongeza wananchi kwa kujitokeza katika uzinduzi huo na amewashauri kutengeneza vibao vya majina ya Mitaa  vyenye majina yao  kwani kutengeneza  vibao hivyo kutawafanya majina yao yaishi miaka yote hata kama wamiliki wa majina hawatakuwepo lakini majina hayo yataendelea kutumika.


 " tengenezeni vibao vyenye majina yenu ili muweke alama ambazo hazitafutika ili ziwe kumbukumbu hata kwa vizazi vinavyokuja" amesema Msanga



Akitoa ufafanuzi wa zoezi hilo Afisa Ardhi wa Wilaya Ndugu  Wickriph Benda amesema zoezi hili linawapa uhuru Wananchi kushiriki kwa kuchagua majina ya Mtaa na anayeweza kutengeneza kibao na kuweka majina ya Mtaa ameruhusiwa lakini majina yanayoruhusiwa niyale yenye maana nzuri, yasiwe ya kejeri na matusi bali yawe majina ya watu au kitu kinachopatikana katika eneo husika ili iwe rahisi kutambulika.


Uzinduzi huo umehudhuliwa na Wananchi, ambao wameona kukamilika kwa operersheni hiyo kutasaidia kujulikana kwa mitaa na hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii na nyingine nyingi.



Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.