• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

Mradi wa Mama na Mtoto kupunguza Vifo vya Akina Mama Wajawazito na Watoto Chini ya Miaka Mitano Wilayani Kwimba.

Posted on: December 8th, 2017

Mradi wa Mama na Mtoto ni mradi  unaofadhiliwa na Serikali ya Canada kwa kishirikiana na  Chuo Kikuu cha  Calgary  pamoja na Chuo Kikuu cha Afya cha Katoliki (CUHAS-Bugando) Mwanza.Lengo kuu la mradi ni kuboresha utoaji wa huduma za muhimu za awali kwa mama mjamzito, wakina mama, watoto wachanga pamoja na watoto walio na umri chini ya miaka mitano na kuboresha namna ya utoaji huduma za afya pamoja na utumiaji wa huduma muhimu za makundi lengwa Wilayani Kwimba.


Akizungumza katika zoezi la  tathimini ya vifaa tiba na vitendea kazi katika hospital, Zahanati na Vituo vya afya wilayani Kwimba Dr. Dismas Matovelo Msimamizi wa mradi wa Mama na Mtoto amesema shughuli za Mradi huo ni pamoja na utekelezaji wa uboreshaji huduma kwa kuzingatia matokeo ikiwemo ukarabati wamiundombinu ya vituo (Majengo,Umeme,, Maji) na ununuzi wa vitendea kazi na vifaa tiba,kujengea uwezo timu za Halmashauri na kamati za vituo katika usimamizi na uendeshaji wa utoaji huduma za afya na kutoa mafunzo, kusimamia na kufuatilia watoa huduma wa afya wa jamii na kufanya kazi na makundi ya jamiiili kukuza na kuboresha namna ya utoaji wa huduma za afya.



Dr. Maendeleo Boniphance  ( Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Bugando) chini ya Mradi wa Mama na Mtoto akikagua Kitanda cha kujifungulia katika Zahanati ya Kiliwi.

Naye Bibi Magdalena Mwaikambo Mwezeshaji kutoka Mradi wa Mama na Mtoto aliwaomba wajumbe wa Kamati ya Afya ya Wilaya kuhakikisha wanashiriki na kusimamia kwa Uthabiti Mradi wa Mama na Mtoto ili uweze kuleta mafanikio chanya kwa  walengwa waliokusudiwa. Aliyasema hayo wakati akiutambulisha Mradi kwa wajumbe wa Kamati ya Afya ya Wilaya 'CHMT"


Bibi Magdalena Mwaikambo Mwezeshaji kutoka Mradi wa Mama na Mtoto akiutambulisha Mradi kwa Kamati ya Afya ya Wilaya ya Kwimba.

Kwa upande wake Bibi Tumsifu Matutu mwezeshaji kutoka kutoka Mradi wa Mama na Mtoto alisema  mradi utaziwezesha kamati za Afya, vituo vya kutolea huduma kufanya usimamizi shirikishi na ushauri katika kuboresha huduma vituoni ilikuboresha ubora wa takwimu na utoaji wa huduma.

 




Bibi Tumsifu Matutu mwezeshaji kutoka Mradi wa Mama na Mtoto akielezea Masuala ya usimamizi shirikishi.

Akichangia  DR. Rose Mjawa Laiser kutoka katika Mradi wa Mama na Mtoto alisema  ili Mradi uweze kufanikiwa suala la  Usawa wa Kijinsia  lazima lizingatiwea Sehemu za kutolea huduma za Afya.




DR. Rose Mjawa Laiser kutoka katika Mradi wa Mama na Mtoto akielezea Masuala ya Usawa wa Kijinsia mahali pa kutolea huduma

Akihitimisha ziara, Dr.  Mtengwa D.M kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji  alieleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba iko tayari kufanya kazi na  Mradi wa Mama na Mtoto kwakuwa takwimu zinaonesha kuwa vifo vya akina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano viko juu ukilinganisha na Halmashauri nyingine za Mkoa wa Mwanza.

Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ina jumla ya hospitali 1 ya wilaya, vituo vya Afya 5 na Zahanati 44 zinazotarajia kunufaika na Mradi wa Mama na Mtoto.



Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.