MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA WILAYANI KWIMBA UKITOKEA MAGU
Posted on: August 28th, 2025
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija apokea Mwenge wa Uhuru kutoka Wilaya ya Magu kwa kuwahakikishia wakimbiza Mwenge usalama wao na chombo pia amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha za miradi ya maendeleo ikiwemo Zahanati na Vituo vya Afya,maji na miundombinu ya Elimu.
" nikuhakikishie kiongozi wa mbio za Mwenge Ndugu Ismail Ally Ussi kuwa leo mtajionea kazi nzuri inayoendelea kutekelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"
Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kilomita 102 na kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi sita yenye thamani ya bilioni 1.5
Pia ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wananchi kuwa leo 28,Agost 2025 ni siku ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi hivyo amewasihi Wananchi kuwa tayari kushiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.