MWENYEKITI APEWA MWEZI MMOJA KUREJESHA FEDHA YA KIJIJI ALIYOTUMIA
Posted on: July 23rd, 2025
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe Ng'wilabuzu Ludigija amemtaka Mwenyekiti wa Kijiji cha Igunguhya Ngudu. Godfrey Singano Salum kurejesha shilingi 500,000 fedha ya kijiji aliyoitumia kwa matumizi yake binafsi
" Mwenyekiti nakupa mwezi mmoja leo ni tarehe 23,Julai 2025 ikifika tarehe 23,Agosti 2025 hiyo fedha ikabidhiwe kwa kijiji la sivyo hatuaza kisheria zitachukuliwa dhidi yako" Dc Ludigija
Haya yametokea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji hicho ambapo Mkuu wa Wilaya alikuwa akisikiliza na kutatua kero za Wananchi.
Mkuu huyo amewasisitiza wananchi wa kijiji hicho kuanzisha ujenzi wa Zahanati kwani wananchi wametoa kero hiyo ya kupata huduma za afya katika vijiji jirani ambako kuna umbali kutoka kijiji hicho.
Pia amewataka wasimamizi wa maji kuhakikisha wanafanya matengenezo ya mabomba mapema pindi wanapopata taarifa ya mabomba kuvuja.
Wananchi wameiomba Serikali kutengeneza barabara za vitongoji ili kuondoa kero inayowapata hasa wanafunzi kufikia shule ya Msingi Kabale
"tunaomba barabara ijengwe ya kutoka nkonze kwenda Shule ya Msingi Igunguhya na barabara ya kutoka Mwasubi kwenda Shule ya Msingi na Sekondari Kabale" amesema Fausti Mathias
Wananchi wamehamasishwa kushiriki uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba " tunzeni vitambulisho ili mwezi wa kumi mkapige kura mchague viongozi watakaohamasisha maendeleo, acheni tabia za kusema fulani atapita harafu hamuendi kupiga kura" Ludigija
Pia amewasisitiza wananchi hasa wanawake kuhudhulia kliniki wanapokuwa wajawazito ili kuepusha vifo vya mama na mtoto vinavyosababishwa na wanawake kutojifungulia hospitali.
Aidha Mkuu wa wilaya amekemea tabia za baadhi ya wananchi kuozesha watoto ambao wanatakiwa kusoma
" ni malufuku kuozesha watoto wadogo hao wanatakiwa waende shule, nawaelekeza watendaji msimamie hili yeyote atakayebainika anaozesha watoto,anawapa kazi za biashara watoto badara ya kuwapeleka shule toeni taarifa"
Naye Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kwimba Deocres Mkandala amewataka wananchi kuacha kufanya ukatili kwa wanawake na watoto, na kutoa taarifa anapobainika mtu anayefanya ukatili kwa watu wengine.