• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

MWENYEKITI KAMATI YA AMANI YA MKOA AWASHAURI WANANCHI KUPUUZA MANENO YANAYOKASHIFU CHANJO

Posted on: October 1st, 2021

Akiongea katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika leo tarehe 01, Oktoba 2021  kwenye uwanja wa Kwideko Ngudu Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza  Askofu Charles Sekelwa amesema Wananchi wanapaswa kupuuza maneno yasiyo na tija yanayojaribu kuhafifisha chanjo ya UVIKO-19 ionekane kuwa haifai na haina faida kwa Wananchi.


Askofu huyo amesisitiza kuwa Amani ya waumini  inapatika tu pale mtu anapokuwa na Afya iliyo salama hivyo amewaasa Wananchi wote kujitokeza kuchanjwa ili kuwa na uhakika wa kinga dhidi ya UVIKO-19 ugonjwa unaosababisha madhara makubwa pindi unapompata mtu asiye na kinga.


Aidha amesisitiza kuwa Wananchi wasiyajali maneno yanayo enezwa kuwa watu wakichanjwa wanapata madhara yanayopelekea magonjwa mbalimbali, amesisitiza kuwa  hayupo kiongozi wa Dini ambaye yuko tayari kuona Waumini wake wanakuwa wagonjwa kutokana na chanjo,


"mimi ni Mchungaji zaidi ya miaka 37 siwezi kuja kudanganya watu kuwa chanjo ina madhara au haina, nimejiridhisha kuwa chanjo ni salama ndipo nikachanjwa na nawahamasisha na nyie mchanjwe, nawasihi ukiona tumeinuka kuja kuwaambia hili ni kwa sababu tuna uchungu na waumini wetu na Nchi yetu pia. Nimesema kama shahidi mtumishi wa Mungu tujiepushe na propaganda zisizo za kweli". amesema Askofu Sekelwa


Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi wa Dini mbalimbali akiwemo Sheikh Mohamedi Moledina ambaye amewataka wananchi kuzitumia Dini vizuri ili ziweze kuleta manufaa kwa Jamii, amesisitiza kuwa Dini zikitumika vizuri zinaweza kuunganisha watu lakini zikitumika vibaya zinatenganisha watu na kuleta madhara makubwa katika Jamii.


Katika Mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robart Gabriel amewashauri Wananchi kuchanjwa chanjo ya UVIKO-19 ili kujihakikishia kinga dhidi ya virusi vya corona na kuona umuhimu wa kuwa na Afya njema ili kuendelea kuzitunza familia zao na kuendelea kulitumikia Taifa. Kutokana na Elimu hiyo iliyotolewa na viongozi Wananchi wamejitokeza kuchanjwa ambapo zoezi la Chanjo limefanyika hapo hapo katika uwanja wa Kwideko.



Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO LA UTAWALA LA HALMASHAURI

    May 18, 2025
  • WAUGUZI WATAKIWA KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA

    May 12, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEIMOSI YAHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU

    May 01, 2025
  • MKURUGENZI AWATAKA WATUMISHI WOTE KUFANYA KAZI KWA UPENDO NA UADILIFU

    April 28, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.