Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Mhe. Thereza Lusangija amewasisitiza waheshimiwa Madiwani kutafuta suluhisho la changamoto mapema pindi zinapojitokeza badara ya kusubiri kuziwasilisha changamoto hizo kwenye baraza.
Amayasema hayo kwenye baraza la Madiwani robo ya tatu ya mwaka 2024/25 siku ya kwanza ambapo taarifa za Kata na Taasisi mbalimbali zimewasilishwa.
Aidha waheshimiwa Madiwani wamemtaka Meneja wa RUWASA kuongeza juhudi katika kuwahimiza wakandarasi wanaojenga miundombinu ya maji Kata ya Nyamilama kukamilisha mradi huo ili kuondoa adha ya upatikanaji wa maji inayowakabiri wananchi wa Kata hiyo
" kila tukiwasilisha changamoto ya huyu mkandarasi majibu ni hayohayo tunataka huu mradi ukamilike Wananchi wapate maji" amesema Diwani wa Kata ya Nyamilama Mhe. Mgelegele
Katika mkutano huo Tanesco wameshauriwa kuzingatia maeneo yenye taasisi na majengo muhimu ya Serikali wanaposambaza umeme kwenye ngazi ya vitongoji ili kufikisha huduma maeneo ya hayo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.