• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

NAIBU KATIBU MKUU BARA CHRISTINA MNDEME AFURAHISHEA NA MRADI WA UJENZI WA KITUO CHA AFYA HUNGUMALWA

Posted on: August 11th, 2022

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Bara Ndugu  Christina Mndeme aipongeza Kwimba kwa kupata miradi ya maendeleo ukiwemo mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya Hungumalwa, ameyasema hayo leo tarehe 11,Agosti 2022 katika Kituo cha Afya Hungumalwa wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo hicho ambapo Kata ya Hungumalwa  ilipokea milioni 500 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Afya.

“ tunaposema Mama Samia anaupiga  mwingi hii ndiyo maana yake tarifa yenu imesema Kwimba  mmepokea bilioni 28 kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ndiyo maana  ukienda kweye sekta ya  Afya unamkuta mama Samia ,barabara unamkuta,maji yupo,Elimu, na miradi mingine  hongereni sana Kwimba”amesema Mndeme


Kiongozi huyo amesisitiza  mwezi wa tisa  kituo cha Afya  Hungumalwa  kiwe kimekamilika na kuanza kutoa huduma, ili lengo la kutoa huduma kwa Wananchi likamilike.Aidha  amewaelekeza  Madaktari na wauguzi kuongeza  uboreshaji wa huduma za Afya ikiwa na lengo la kupunguza vifo vinavyowezekana kuepukika

“ niwaombe sana wauguzi na madaktari mboreshe huduma za Afya, mgonjwa anapokuja hospitali apate matumaini ya kuishi siyo wagonjwa wanafika hospitali wanakosa matumaini, toeni huduma bora” amesema Mndeme


Akiongea na viongozi na Wananchama wa Chama Cha Mapinduzi katika Tawi la Malya na Ngudu, Mndeme  amewataka viongozi wa Chama na Serikali kufanya kazi kwa bidii ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ili adhima yake ya kufikisha maendeleo kwa Wananchi itimie.


Aidha kiongozi huyo  amesisitiza  upandaji wa miti  inayovumilia ukame na hali  ya hewa ya  Kwimba, miti itakayosaidia kuzuia upepo mkali unaoweza kuezua mapaa ya majengo, lakini miti itaweza kuyafanya mazingira yawe na muonekano mzuri.

Akihitimisha hotuba yake ametoa Elimu ya Sensa, amewashauti  wananchi wote kuwa tayari kuhesabiwa ifikapo tarehe 23,Agosti 2022 .

Naye Mkurugenzi wa Halmashairi akisoma taarifa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ikiwemo miradi ya Afya, Elimu, maji, barabara, umemena mingine



Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.