Leo historia imeandikwa kwa Wananchi wa Mkoa Mwanza na Tanzania kwa ujumla kwani daraja lenye urefu wa kilomita 3 ambalo ni la kwanza kwa ukubwa Afrika Mashariki na Kati limezunduliwa leo 19, Juni 2025 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan
" leo kwa mara ya kwanza tumefungua daraja la JP Magufuli ambalo ni kubwa la kwanza Afrika Mashariki na Kati, ile hadidhi ya kusikitisha ya Mheshimiwa Marehemu Magufuli ya kushindwa kuvuka na mtumbwi kupeleka Posa ndio iliyomfanya aone umuhimu ujenzi wa daraja hili ili kuokoa maisha ya watu waliokuwa wakipoteza maisha kwa kuzama na boti, pia kupoteza muda leo tumetimiza adhmma yake" amesema Rais
Mheshimiwa Rais amesema ujenzi wa daraja umekamilika na lengo limekamilika wananchi na wafanya biashara wote tutanufaika na daraja hili.
Amesisitiza kuwa daraja hili limekuwa fursa kwa wote walioshiriki ujenzi wa daraja hilo pia amewapongeza wote walioshiriki ujenzi huo.
Mheshimiwa Rais amewaasa vijana wote walioshiriki ujenzi na watumiaji wote kutumia vizuri na kulienzi daraja hilo na kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara ili kukuza biashara na Nchi jirani kama Burundi, Rwanda na wengine.
Amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kujipanga kulinda daraja hilo kwani litatumika kwa watu mbalimbali wa Afrika mashariki hivyo usalama unatakiwa uwe wa uhakika.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo waziri wa Ujenzi Abdalah Ulega amesema jumla ya bilioni 718 zimetumika kujenga daraja hilo lenye hadhi kubwa
" kukamilika kwa daraja hili kunaenda kurahisisha usafiri na hivyo kuchochea na kukuza biashara, pia wakulima,wavuvi, wafugaji sote tutanufaika na daraja hili, tunakushukuru Mheshimiwa Rais kwa kusimamia na kukamilisha daraja hili" amesema Ulega
Wananchi wameipongeza Serikali kwa ujenzi wa daraja hilo kwani itasaidia kuondoa na kupunguza upotevu wa muda uliokuwa unatumika kuvuka katika vivuko vya kigongo - busisi
" nitumie nafasi hii kuipongeza Serikali kwanza kwa kujenga daraja hili llenye hadhi ya nyota tano lakini hili daraja litatusaidia kuondoa changamoto ya kupoteza muda sasa ni dakika nne tu kuvuka" Belnad Dott