• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

RC MAKALLA AMTAKA MKANDARASI KUKAMILISHA JENGO LA UTAWALA KABLA YA DISEMBA 30

Posted on: November 28th, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos  Makalla amemtaka Mkandarasi Kwiyera Interprises Limited kukamilisha ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kufikia Disemba 30,2023 ili awamu zingine za ujenzi ziendelee na kuwapatia watumishi na wananchi huduma nzuri.


Ametoa agizo hilo mapema leo akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kwenye wilaya ya Kwimba alipotembelea ujenzi huo unaofanyika kwenye kata ya Ngudu kwa zaidi ya Bilioni 4 ambapo bilioni 1.3 zitatumika kwa awamu ya kwanza.


"Mkandarasi leo umechelewa na umeshaongezewa mara nne muda wa kukamilisha nami kwa kuzingatia ucheleweshaji wa malipo ya fedha kwa mkandarasi huyo nakutaka sasa ukamilishe jengo hili hadi disemba 30 mwaka huu."


Aidha, Makalla amemshukuru Rais Samia kwa kutenga fedha zaidi ya Bilioni 4 kwa ajili ya Ujenzi wa jengo hilo (Bilioni 1.3 awamu ya kwanza) ambapo amebainisha kuwa litasaidia kuwaweka watumishi kwenye mazingira nadhifu ya kufanyia kazi na wananchi kupata huduma nzuri.


Awali Mkuu wa Wilaya ya kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija alifafanua kuwa Mkandarasi huyo amekua na mwenendo wa kusuasua kwenye ujenzi hadi kufikia hatua ya kuongezewa muda kwa mara tatu baada ya muda wa awali kuisha kwa mujibu wa mkataba pamoja na kupatiwa fedha.


Akikagua hali ya utoaji huduma kwenye  Hospitali ya Wilaya iliyojengwa kwa zaidi ya Bilioni 4 kwenye eneo la Icheja kuanzia mwaka 2018/19 CPA Makalla amewapongeza Kwimba kwa kukamilisha ujenzi ambapo wagonjwa zaidi ya 475 wanalazwa kwa mwezi na kusaidia mtiririko wa huduma.


"Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha za ujenzi na vifaa vya kisasa, tunatambua kazi nzuri inayofanywa na wataalamu wa afya ila lazima tusimamie matumizi ya lugha nzuri  kwa wagonjwa kwani inaleta matumaini hata kabla ya kuanza kutoa huduma yenyewe" Amesisitiza CPA Makalla.


Akitoa taarifa ya Ujenzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Happness Msanga amebainisha kuwa fedha hizo zilitoka kwa ajili ya ukarabati wa iliyokua hospitali ya wilaya eneo la kakora lakini kutokana na ufinyu wa eneo waliamua kujenga hospitali mpya.


Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.