• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

RC MJALA ATAKA ELIMU YA ATHARI ZA UTORO SHULENI ITOLEWE

Posted on: July 27th, 2023



Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA. Amos Makala amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Kwimba na uongozi wa Halmashauri ya Kwimba  kuhakikisha wanasimamia na kutoa elimu kwa wazazi na jamii kwa ujumla juu ya umuhimu wa elimu kwa watoto ili kutokomeza suala la utoro na kukuza ufaulu shuleni.


"Swala la utoro shuleni, ufaulu na watu kutokumaliza shule niwaombe sana watendaji wetu tutoe elimu hiyo ya umuhimu wa watoto wetu kusoma na kuhakikisha ni ajenda yetu sote na sio afisa elimu tu na jamii nzima ielewe umuhimu wa kuwapeleka watoto shule kwa kuwa Serikali ya awamu ya sita imeboresha miundombinu ya elimu hakuna sababu ya watoto kutokwenda shule," amesema  Makalla.


Mhe.Makalla amesema hayo leo Juni 27, 2023 kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwa ajili ya kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) za Mwaka 2021/22.


Aidha Mkuu huyo amewataka viongozi wa Wiaya ya Kwimba  kutafuta suluhu katika Ukusanyaji wa ushuru kwa wafanyabiashara waliojenga vibanda katika stendi ya Ngudu na Malya.


"Niwaombe mkae nao muwaeleze kwamba eneo lile ni la serikali na wanachotakiwa kufanya na mkuu wa wilaya uongoze kikao hicho, muwabaini wachochezi wa mgogoro ambao hawahusiki na eneo hilo mkae katika majadiliano na watu wanaohusika na vile vibanda, mpate orodha ya watu waliokubali kusaini mikataba na kulipa na mpate  orodha ya watu waliogoma kulipa," RC Makalla.


Vilevile, Mhe. Makalla ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwa kupata Hati Safi kutoka kwa Mdhibiti na  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na amewataka Madiwani kufanyia kazi na kuijadili taarifa ya mkaguzi mara kwa mara.


Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija amemuahidi Mkuu wa Mkoa kwa niaba ya watumishi, kamati ya usalama na Kwimba kwa ujumla kwamba watasimamia maelekezo yote aliyoyatoa.


Halikadharika, Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Mkoa wa Mwanza Waziri Shabani kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amesema Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imepata hati safi inayoridhisha kutokana na ushirikiano alioupata kwa watumishi wa Halmashauri hiyo.

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.