• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

RC MTANDA AAGIZA KUFUNGWA MFUMO WA KUKUSANYA MAPATO ILI KUDHIBITI UPOTEVU WA MAPATO

Posted on: September 14th, 2024


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amemuagiza Katibu Tawala Mkoa kushirikiana na Mganga Mkuu wa Mkoa kuhakikisha ndani ya siku 14 wanaweka mfumo wa makusanyo na matumizi ya fedha kwenye Kituo cha Afya Budushi kilichopo kata ya Sumve wilayani Kwimba.


Ametoa agizo hilo mapema leo septemba 14, 2024 wakati akifanya ukaguzi wa huduma za afya kwenye kituo hicho na kubaini kuwapo kwa mfumo wa makusanyo na matumzi wa makaratasi badala ya Mfumo wa kisasa wenye ufanisi na unaodhibiti upotevu wa mapato (GOTHoMIS).


Aidha, ametoa rai kwa Mganga mkuu wa wilaya hiyo kuwa mbunifu na mwenye maamuzi ya haraka katika kufunga mifumo na vifaa tiba na visaidizi kwenye vutuo vya kutolea huduma ili malengo ya serikali ya kuboresha huduma za afya yaonekane mapema.


Akikagua ujenzi hususani kwenye jengo la Mama na Mtoto na kichomea taka ameagiza kasi ya ujenzi iongezwe ili hadi kufikia septemba 30, 2024 wakamilishe na huduma kwa wananchi zaidi ya elfu 17 ziendelee kutolewa katika hali ya ubora na kuwapunguzia msongamano kwenye hospitali ya Kanisa waliyokua wanapata huduma siku za nyuma.


Awali, akiwasilisha taarifa Mganga mfawidhi wa Kituo hicho Paul Kanga amesema mradi wa ujenzi wa kituo hicho umepokea kiasi cha Tshs. 656.4 milioni ambapo Tshs. 300 Milioni kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri na Tshs. 356.4 kutoka TASAF na wananchi wamechangia fedha milioni 8 kwaajili ya kununua eneo hilo.


Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa  amekagua miradi mingine ikiwemo mradi wa upandaji miti Shule ya Sekondari  Walla,mradi wa ujenzi wa maduka ya biashara  sokoni Ngudu na ujenzi wa madarasa kumi Shule ya Sekondari  Ngudu na ujenzi wa barabara ya lami Ngudu.

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.