Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka Wananchi kutunza miundombinu ya maji ili kujihakikishia upatikanaji wa maji safi na salama,pia amewataka RUWASA kuwashirikisha wananchi katika kupanga bei za maji ili kuwajengea umiliki wa miradi
Ameyasema hayo leo 28,Julai 2025 wakati akikagua utekelezaji wa miradi yamaendeleo ikiwemo mradi wa ujenzi wa tenki la Maji katika Kijiji cha Maligisu ambapo mradi umefikia asilimia 90 ya ukamilishaji.Mtanda amewahamasisha wananchi kuvuta maji katika nyumba zao ili kunufaika na mradi huo.
Mkuu huyo amekagua maendeleo ya ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari Ngudu,ujenzi wa vyumba vya biashara soko la zamani Ngudu,ujenzi wa nyumba za wakuu wa Idara wa Halmashauri na ujenzi wa daraja ambapo amewaelekeza wasimamizi wa miradi hiyo kuongeza kasi ili miradi ikamilike kwa wakati na ianze kutoa huduma.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa amekagua matumizi ya nishati safi ya kupikia katika Shule ya Sekondari Ngudu ambapo amewapongeza kwa hatua hiyo ambayo awali kabla ya matumizi ya nishati safi walitumia 2,700,000 kwa mwezi kwa matumizi ya kuni lakini baada ya kuanza kutumia nishati safi wanatumia gharama ya 1,600,000 ambapo wameweza kupunguza ghalama za matumizi ya nishati.
Baada ya kukagua mradi huo Mheshimiwa Mtanda amemuelekeza Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza kuhakikisha shule zote za bweni wanaanza kutumia nishati safi ya kupikia ili kutunza mazingira na kupunguza ghalama za uendeshaji wa shule
" kama hapa Ngudu sekondari wameweza na shule nyingine waanze kutumia nishati safi,kwanza itasaidia kutunza mazingira na kupunguza kukata miti ovyo" Mtanda