• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

RC MTANDA AZUNGUMZA NA WAZEE WA KWIMBA AWAAHIDI KUMALIZA KERO ZA MAJI

Posted on: June 14th, 2024

RC MTANDA AZUNGUMZA NA WAZEE WA KWIMBA AWAAHIDI KUMALIZA KERO ZA MAJI NA BARABARA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda amesema serikali ipo mbioni kumaliza kero ya Maji kwa wananchi wa Ngudu na wote wilayani Kwimba kwa kujenga mradi mkubwa pamoja na kuharakisha uwekaji Lami kwa kilomita 3 za Mjini na baadae kupeleka hadi Mabuki.


Mhe. Mtanda ametoa ahadi hiyo leo tarehe 06 Juni, 2024 wakati akizungumza na Wazee wa Kwimba katika kikao chake kifupi alichoketi nao kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.


"Leo nimefanya kazi kama ya Tomaso maana nimeona na kuamini kuwa Ngudu na Kwimba kwa ujumla wanapata adha ya barabara na nawaahidi tutaanza kujenga hizo Kilomita 3 za hapa na baadae tutatafuta fedha ili kuunganisha Kilomita zote 26 hadi barabara kuu kule Mabuki", amesema Mhe. Mtanda.


Aidha, ametoa wito kwa vituo vya afya, zahanati na Hospitali ndani ya Wilaya hiyo na zingine kuhakikisha wanatoa upendelea kwa wazee kwa kuimarisha madirisha ya kuhudumia wazee wanapofika kwenye vituo hivyo kupata huduma za afya.


Mkuu huyo ametumia kikao hicho kuwaasa wazee kuhakikisha wanasomesha watoto wa kike "Watoto wa kike wapewe fursa ya kusoma, ni uwekezaji mkubwa kuliko kupokea ng'ombe wa mahari, tuwaache wasome ili baadae wawe madaktari wazuri na waweze watusaidie" amesisitiza Mkuu wa Mkoa.


Naye, Mzee Edward Seneda Mwenyekiti wa Wazee Kwimba ameelezea furaha yake kwa kupata fursa ya kuzungumza na Mkuu wa Mkoa na kueleza changamoto zao na kuzichukua kwa ajili ya kuzifanyia kazi siku za usoni.


Shekhe wa Wilaya na Kiongozi wa Kamati ya Amani na Kiongozi wa Sungusungu wametumia wasaa huo kushukuru Serikali ya wilaya kwa kuwajali na kushirikiana nao kwenye shughuli mbalimbali na wamemtakia Mkuu wa Mkoa kheri katika shughuli zake.

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.