Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka wakulima wa pamba mkoani humo kung'oa na kuchoma moto mazalia ya Pamba ya msimu uliopita kabla ya Septemba 15 ya kila mwaka ili kutoathiri msimu mpya wa kilimo hicho.
Mhe. Mtanda ametoa agizo hilo mapema leo Jumatat Novemba 18, 2024 wakati akifunga kikao cha viongozi ngazi ya wilaya kwa ajili ya kampeni ya ung'oaji wa masalia ya Pamba wilayani Kwimba.
Amesema kutofanya hivyo kunasababisha wadudu kuzaliana na kusubiri pamba mpya shambani kuiharibu, hivyo ili kujihakikishia uzalishaji wenye tija ni lazima wakulima wafuate kanuni za kilimo cha zao hilo kwa kusafisha mashamba mapema kabla ya msimu mwingine.
"Viongozi wote mpo hapa maafisa ugani, tarafa, kata na vijiji nawaagiza muda wa hiyari umekwisha twendeni tukatekelze kanuni bora za kilimo cha Pamba kwani zao hili ndio injini ya uchumi wa wananchi wa Mwanza kwa miaka mingi." Mtanda.
Aidha, ameipongeza bodi na kwa kipekee balozi wa Pamba nchini,Aggrey Mwanri kwa juhudi zake za uelimishaji wakulima wa Pamba nchini na kwa kipekee mkoani Mwanza ambako kimsingi amechagiza uzalishaji na kufanya idadi ya wakulima waliopo mkoani humo kuwa sawa na waliopo kwenye mikoa 17 nchini.
Balozi wa Pamba Mhe. Agrey Mwanri amesema tatizo kubwa linalokwamisha Mbegu mpya kumea kwenye mashamba ya Pamba ni wakulima kutong'oa maotea ya pamba ya msimu uliopita kwani msimu mpya unachelewa na hatimaye mvua za vuli zinawapita.
Amefafanua kuwa mwisho wa kusafisha pamba ni tarehe 15 Septemba, 2024 ya kila mwaka ili msimu mpya uanze lakini wapo baadhi ya wakulima wamekua wakiacha maotea kwa lengo la kulisha mifugo kinyume na kanuni za kilimo bora na kupelekea kukwamisha uzalishaji.
"Mkiruhusu mimea ya msimu uliopita kuendelea kubaki shambani mtakua mnakaribisha wadudu kama Chawajani, Kandambili na ndio maana hivi sasa neema na baraka ya zao la pamba kwenye uchumi wa wananchi zimepungua kutokana na kushuka kwa takwimu za uzalishaji." Mwanri.
Aidha, amekemea tabia ya wakulima kuchanganya mazao na akatoa mfano wa Pamba na Mahindi yakioteshwa kwenye shamba moja yanasababisha zao moja kushiba rutuba.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.