RC Mwanza Mhe.John Mongela atembelea miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa chuo cha veta katika kijiji cha Kilyaboya kata ya Ngudu,hapo ameshauri ujenzi uzingatie ubora unaotakiwa ili majengo yaweze kutumika kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Aidha katika ziara hiyo RC amekagua mradi wa ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita milioni 2 ambalo limefikia asilimia 85% kukamilika,tenki hilo likikamilika litaondoa tatizo la maji kukatika katika mji wa Ngudu na maeneo ya jirani.
Katika ziara hiyo Mhe.Mongela amekagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya eneo la Icheja na kuwataka viongozi na wasimamizi kuongeza kasi ya ujenzi ili majengo yakamilike kwa wakati.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.