'Tunatoa pole kwa wanafunzi wote waliopata changamoto ya kuungua mabweni yao kidato cha kwanza na kidato cha tatu, Serikali kupitia vyombo vyake vya usalama inaendelea kuchunguza chanzo cha moto"
Haya yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Bi. Johari Samizi ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika tukio hilo, ambapo wanafunzi wameendelea kuhamasishwa na kutiwa moyo kutokana na janga la moto lilitokea katika Shule ya Sekondari Sumve ambapo mabweni mawili yaliteketea kwa moto tarehe 20,Novemba 2025
Mheshimiwa Johari ametumia wasaa huo kuwapongeza wananchi wa Sumve kwa moyo wa utu waliouonyesha siku hiyo ya tukio ambapo wananchi walihakikisha hakuna mwanafunzi anayezurika na moto
" tunawashukuru sana Wananchi wa Sumve mlionyesha moyo wa utu,watu walihatarisha maisha yao wakaingia kwenye moto kuokoa vitu vya wanafunzi, asanteni sana na niwaombe muendelee na moyo huo wa upendo na kujali" amesema Johari
Naye katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndugu Elikana Balandya ametumia nafasi hiyo kuwapa pole wanafunzi wote waliopata changamoto na amewashauri wasikate tamaa badara yake wawe wastahimilivu na walipokee hilo kama changamoto ambayo haiwezi kuwaharibia taratibu zao za masomo.
Aidha Balandya amewahakikishia wanafunzi hao ulinzi wa uhakika, hivyo wanapaswa kuendelea na masomo yao huku changamoto za vifaa na vitu vyote vilivyoungua vikiendelea kupatiwa ufumbuzi.
Aidha Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Komenkesha ameushukuru uongozi wote kuanzia ngazi ya Mkoa hadi kijiji kwa kuendelea kusaidia kuimarisha ulinzi na kusaidia upatikanaji wa vifaa muhimu vya wanafunzi kama shuka,miswaki, kalamu na vifaa vingine.
Viongozi waliofika shuleni hapo wameahidi kutoa magodoro ya wanafunzi wote waliopata changamoto ya kuungua mabweni yao ili kuhakikisha wanafunzi hao wanalala vizuri na kupata muda wa kupumzika ili janga hilo lisiathiri muda wao wa kujisomea.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.