SHIRIKA LA VIA AVIATION LATOA MICHE YA MITI LAKI MOJA KWIMBA
Posted on: February 4th, 2025
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija awelipongeza shirika la VIA AVIATION kwa kutoa miche ya miti 100,000 kwa lengo la kuunga juhudi za Serikali za kutunza mazingira na kuepukana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
"Niwashukuru shirika la VIA AVIATION kwa kutoa miti 100,000 na hapa wametanguliza miche 1500, mmefanya kazi kubwa sana na Wilaya ya Kwimba tunaendelea na utaratibu wa kupanda miti ambapo zaidi ya miti laki saba imeshapandwa maeneo mbalimbali kwenye taasisi na maeneo mengine, tuwaombe muendelee kuleta miti ili tubadirishe Kwimba yetu iwe ya kijani" Ludigija
Mkuu huyo amewataka Walimu na wanafunzi kusimamia miti iliyopandwa ili ikue na lengo la kuhifadhi mazingira litimie. Pia amemuomba Mkurugenzi wa shirika hilo kuendelea kuleta miche ya miti ya matunda na mbao ili wananchi waendelee kupanda hatimaye Kwimba iwe ya Kijani.
Akikabidhi miche hiyo Mkurugenzi wa shirika la VIA AVIATION Bi. Susan Mashibe ameahidi kuendelea kushirikiana na Wilaya ya Kwimba katika utunzaji wa mazingira kwa kutoa miti mingi zaidi pale itakapohitajika " mimi ni jamii ya kifugaji kwahiyo najua tunapenda kukata miti kwahiyo tumeona tuanze na Kwimba Hungumalwa pia tunajua ndege zinaharibu mazingira hivyo tumeona ni vyema kupanda miti ili kulinda mazingira yetu"
Aidha Mkurugenzi huyo amewashauri wanafunzi kupenda masomo na kuongeza juhudi katika masomo ili waweze kutimiza ndoto zao kama yeye alivyokazana katika masomo hadi akawa Rubani.
Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Hungumalwa amelishukuru Shirika hilo kwa kuona umuhimu wa kupeleka miti shuleni hapo " tunaishukuru hii taasisi kwa kuichagua Shule yetu kuwa eneo la uzinduzi wa program yao ya kupanda miti Wilayani Kwimba" Kudera