Mkurugenzi wa mipango na sera kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Ndugu John Mihayo Cheyo ameipongeza shule ya Sekondari Bupamwa kwa kuongeza hali ya ufaulu wa kidato cha nne na kufuta ziro.
Ameyasema hayo kwenye mahafari ya 15 ya Kidato cha nne iliyofanyika tarehe 7,Septemba 2024 Shuleni hapo
" niwapongeze walimu,wanafunzi na viongozi wote mlosimamia uboreshaji wa elimu hadi kufikia kufuta ziro kwa matokeo ya kidato cha nne sasa ongezeni juhudi muondoe daraja la nne" alisema Cheyo
Akiwasilisha taarifa ya shule hiyo Mkuu wa Shule Mwalimu Herman Shingisha alisema Pamoja na mafanikio makubwa ya kupandisha ufaulu shule hiyo bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa matenki ya kutunzia maji, bwalo,jengo la utawala,jengo la TEHAMA na mahitaji mengine.
Ndugu Cheyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Mahafali hiyo alitatua baadhi ya changamoto za Shule hiyo kama matenki ya maji na sufuria za kupikia chakula cha wanafunzi.
Jumla ya wanafunzi 92 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne kati ya wanafunzi 202 walioanza kidato cha kwanza mwaka 2021, ambapo changamoto kubwa katika shule hiyo ni wanafunzi kuacha shule, utoro wa rejareja na wengine kuhama
" tatizo kubwa lililokuwa linasababisha wanafunzi wetu kuacha shule ni umbali maana wapo wanafunzi wanaotembea zaidi ya kilomita 40 kuja na kurudi nyumbani, lakini tatizo limetatuliwa maana shule imeshajengwa huko Kiliwi ambayo inachukua wanafunzi wanaotoka kijiji cha kiliwi, Itegamatu na kijiji cha Dodoma" alisema Mkuu wa Shule Shingisha
Nao wanafunzi wanaotokea vijiji hivyo walieleza jinsi walivyopambana na changamoto hasa kipindi cha masika ambapo mito ikijaa maji walishindwa kufika shuleni " tumepitia wakati mgumu sana maana kutoka nyumbani hadi hapa shule ni mbali sana na kipindi cha mvua kuna mto ambao ukijaa haiwezekani kupita kuja shuleni lakini nimepambana, wazazi walinipa baskeli ambayo ilinisaidia" alisema Justina Kasangu
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.