Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe Ng'wilabuzu Ludigija amewataka wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kwenda kutumia mikopo iliyotolewa kwa malengo yaliyokusudiwa ili waweze kuinuka kiuchumi na hasa amesisitiza kuwa Serikali inataka wanawake wamiliki uchumi kupitia mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri.
Aidha amewasisitiza vijana waliopata mikopo kwenda kujikita kwenye biashara ili maendeleo yaonekane katika maeneo wanayoishi, pia amewataka kuhakikisha faida wanayopata wanaiendeleza ili biashara zao zikue zaidi.
Amesisitiza kuwa fedha hiyo siyo hisani bali ni mkopo hivyo ni lazima kurejeshwa Halmashauri ili na watu wengine waweze kupata mikopo hiyo
Pia amewataka kuepuka ushauri mbaya ambao unaweza kupelekea wote waliopata mikopo kushindwa kutimiza yale yaliyokusudiwa
" unajua fedha inaushawishi msije mkabadirisha mpango kutokana na ushawishi kutoka kwa watu, kafanyeni biashara mlizopanga kufanya"
Pia amewataka kuwa waaminifu katika kurejesha mikopo hiyo ili watu wengine ambao bado hawajapata mikopo waweze kupata
hii ni mikopo isiyo na riba ni tofauti kabisa na mikopo mingine maana hii haina riba kwahiyo itumieni mikopo hii kwenda kutimiza malengo mliyopanga"
Aidha amewataka wanawake waliopata mikopo hiyo kutokabidhi fedha kwa wenza wao badara yake wakafanye biashara ili waweze kujipatia kipato
"tunajua kunawanawake wanachukua mikopo hii kwa migongo ya waume zao msifanye hivyo, kwenye fedha hakuna kuaminiana, fedha mnayopewa mkafanye biashara ili muweze kurejesha kwa wakati"
Akiwasilisha taarifa ya mikopo hiyo Kaimu Mkuu wa Idara ya maendeleo ya Jamii Wivina Biyabato amesema jumla ya vikundi 18 vimekidhi kupewa mikopo ambapo wanawake ni vikundi 10, vijana vikundi 5 na walemavu vikundi vitatu ambapo jumla ya shilingi 119M zimetolewa kwa vikundi hivyo.
Pia amewataka wote waliopata mikopo kwenda kuwa mabalozi kwa watu wengine ili waweze kuona umuhimu wa kuomba mikopo hiyo kwa maendeleo yao.
Nao wanawake,vijana na watu wenye ulemavu waliopata mikopo hiyo wameahidi kwenda kufanya biashara na kuendeleza ujasiliamari, pia wameahidi kurejesha fedha hizo kwa wakati.



Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.