• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Umefanya Ziara ya Kutembelea Kituo cha Afya Kahangala na Karume

Posted on: January 8th, 2018

Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba umefanya ziara ya kutembelea kituo cha Afya cha kutolea huduma Kahangala kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Magu pamoja na kituo cha afya cha kutolea huduma Karume kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela tarehe 6 Januari, 2018  lengo likiwa ni kupata uzoefu wa matumizi ya Fedha  zilizotumwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa ajili ya ukarabati au ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za Afya.

Akiongea katika ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Ndg Lutengano George Mwalwiba, aliushauri Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kuhakikisha unafuta muongozo uliotolewa na  Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi hiyo ikiwa ni pamoja na matumizi ya  “ Force Account” ili kupunguza gharama na kuongeza ubora wa majengo.

Ndg Mwalwiba aliendele kusema   ni vizuri kumshirikisha Mganga Mkuu wa Mkoa katika hatua zote  ili kuepusha  mkanganyiko katika utekelezaji wa Mradi.

Kwa upande wake Ndg Joel Ally mjumbe wa kamati ya Afya katika Zahanati ya Kahangala alisema  kamati ya Afya ndiyo moyo wa mradi  wajumbe wanatakiwa kujitoa na kuwa na moyo wa kujituma ili mradi uweze kutekelezeka katika hali ya ubora na viwango vilivyokusudiwa.

Akiendelea kuchangia Ndg Mwalwiba alimuomba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kuhakikisha anawandikia barua za uteuzi wasimamizi wa Mradi ili kila mtu atakayezembea  awajibishwe katika eneo lake.




Baadhi ya Majengo ya kutolea huduma katika kituo cha Afya Kahangala Wilayani Magu

Kwa kuongezea Ndg Mwalwiba alisema pamoja na ujenzi wa Wodi ya akinamama, Maabara, Chumba cha kuhifadhia maiti, Jengo la Upasuaji, Matundu Manne ya choo na ujenzi wa Nyumba moja ya Mtumishi. Pia Halmashauri ya Wilaya ya Magu  imejipanga kufanya ukarabati  katika nyumba za watumishi .



Wodi ya kinamama kaika kituo cha Afya Karume Manispaa ya Ilemela

Akizungumza katika Ofisi yake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela Ndg John Paul Wanga alieleza jinsi matumizi ya “Force Accont” yalivyoleta Manufaa makubwa katika utekelezaji wa  Ujenzi wa  kituo cha Afya Kanyerere.

“Force Account  imetupa manufaa makubwa ni pamoja na kupata majengo imara kwa kutumia mafundi watu, tumetengeneza ajira kwa wananchi na kazi imekamilika kwa wakati”


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela Ndg John Paul Wanga akiongea na Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.

Kwa upande wake  Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon amewapongeza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mbili kwa moyo wa kujitolea katika kutekeleza miradi ya serikali na amewaomba wasichoke pindi wataalamu wa ujenzi watakapokuja  kujifunza kwa awamu ya pili. 

Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imepokea kiasi cha Shillingi Millioni Mianne  400,000,000/= kwa ajili ya kutekeleza Ukarabati au  Ujenzi wa  Kituo cha  Afya Malya ikiwa ni lengo la Serikali la kutekeleza mkakati wa kuviboresha na kujenga vituo vya kutolea huduma za afya nchini ili viweze kutoa huduma bora  inayoendana na mahitaji halisi ya wananchi.

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.