Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Bi. Felister Mdemu amevitaka vikundi vya wanawake wajasiriamali wanaonufaika na mikopo ya asilimia kumi ya Halmashauri kufanya kazi kwa ushirikiano.
Ameyasema hayo leo Agosti 20,2024 katika kikao alichokifanya na kikundi cha Upendo na Jikomboe vya Nyambiti
"niwapongeze kwa kazi kubwa mnayoifanya sikutarajia kukutana na wajasiriamali wengi hivi, fanyeni kazi kwa ushirikiano na maturajio yangu nikirudi huku muwe na mitaji mikubwa " amesema Felister
Kiongozi huyo amewashauri wanawake hao kujihusisha na kila jambo linaloweza kuwaletea maendeleo, amewataka kufanya kazi tofauti tofauti siyo wote kujikita kwenye kazi moja ya upishi na upambaji.
Awali akiwasilisha taarifa Afisa maendeleo ya Jamii(W) Bi. Rozalia Magoti amesema Halmashauri inaendelea kutenga asilimia kumi za mapato ya ndani ambapo milioni 299.7 zimetengwa kwaajili vikundi kukopeshwa.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba Ndugu Mohamed Mtulyakwaku amevishauri vikundi hivyo kujiunga kwenye mfumo wa manunuzi wa Nest ili waweze kuomba kazi za upishi kwenye matukio mbalimbali ya Halmashauri.
Wanawake hao wamewashukuru viongozi hao na wameomba mikopo ya asilimia kumi ianze kutolewa ili waombe maana wanayo malengo ya kuongeza mitaji na kukuza biashara zao.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.