• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

VIONGOZI WA VIJIJI WATAKIWA KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO

Posted on: October 11th, 2022


Wenyeviti wa Serikali ya vijiji wametakiwa kusimamia miradi ya maendeleo kwa weledi na umakini wa hali ya juu ili kukamilisha miradi kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

Haya yamejiri katika kikaokazi cha wenyeviti  wa vijiji kilichofanyika leo tarehe 11, Oktoba 2022 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ngudu. Katika kikao hicho viongozi hao wa vijiji wamepata maelekezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na namna bora ya kufanya kazi kwa kuzingatia mipaka na wajibu wa kiongozi.

Aidha katika kikao hicho taatifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo imewasilishwa na Afisa Mipango  Ndugu Rogatevane John Kipigapasi huku akisisitiza ushirikiano wa viongozi wa vijiji katika kuhakikisha miradi inayotekelezwa kwenye vijiji vyao inatekelezwa na kukamilika kwa wakati.Afisa huyo amesema Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imepokea zaidi ya bilioni  nne kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya ujenzi wa madarasa 112 katika Shule za Sekondari ambayo yataghalimu bilioni 2.24

“ niwaombe viongozi wa vijiji mkasimamie mradi huu wa madarasa kwani yanatakiwa kukamilika kabla ya Disemba 15 kwahiyo bila usimamizi mzuri na waushirikiano hatutaweza, hivyo tushirikiane kusimamia, kila mtu afanye kazi kwa nafasi yake” amesema Kipigapasi

Afisa mipango akiwasilisha taarifa hiyo amewataka viongozi wa vijiji kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa ushuru wa mazao pale inapobidi kulipa amesema kutorosha mazao ni makosa makubwa yanayoisababishia Halmashauri ishindwe kukusanya fedha zinazoweza kuongeza maendeleo katika Wilaya ya Kwimba.

Pia amewasisitiza viongozi hao kwenda kutoa Elimu kwa vijana kuhusu umuhimu wa kukopa mkopo usio na riba wa Halmashauri,” Halmashauri inatarajia kukopesha vijana, wanawake na watu wenye ulemavi zaidi ya milioni 200 kwahiyo waambieni vijana waunde vikundi waje wapewe mikopo wakafanye kazi zakuwaongezea kipato” amesema Kipigapasi

Katika kikao hicho ameshiriki Afisa Kilimo Magreth Kavalo ambaye ametoa elimu ya kilimo na maandalizi ya mashamba kwaajili ya msimu wa wakilimo unaoanza sasa “ kulingana na utabiri wa hali ya hewa mvua haitakiwa nyingi kama mwaka jana kwahiyo naomba muwaambie wananchi waandae mashamba mapema, wawe tayari kulima mazao ya aina zote yakiwemo yale yanayostahimili ukame,vilevile niwaombe wakulima ambao bado hawajasajiliwa wafanye  usajili ili wapate urahisi wa kupata mbolea kwa bei nafuu  ukilinganisha na bei iliyoko sokoni mfano mbolea inauzwa 136,000 lakini mkulima aliyesajiliwa anauziwa kwa 70,000” amesema  Mhandisi Kavalo

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Ndugu Denis Kabogo akihitimisha kikao hicho ametoa ufafanuzi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo huku akiwasisitiza viongozi hao kwenda kusimamia miradi yote inayotekelezwa katika vijiji vyao . Pia amewataka viongozi hao kwenda kuhamasisha ujenzi wa vyoo bora katika kila kaya  “ kahamasisheni ujenzi wa vyoo bora kwa kila Kaya na muwaambie wananchi ukaguzi utafanyika watakaokutwa hawajajenga Choo bora watatakiwa kulipa faini ambayo itaanzia 50,000 na kuendelea” amesema Kabogo

Wenyeviti  walioshiriki kikao hicho wameushukuru  uongozi wa Halmashauri kwa kuona umuhimu wa kufanya kikao na wameomba vikao vya namna hiyo vifanyike marakwamara ili wapate nafasi ya kuwasilishwa hoja zao kwa viongozi.







Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.