Viongozi wa vyaama vya siasa na viongozi wa dini washauriwa kuwahamasisha wananchi kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa kuwachagua viongozi bora watakaohamasisha maendeleo na usalama.
Haya yamejiri kwenye kikao kilichofanyika leo Oktoba 31,2024 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ambapo msimamizi wa uchaguzi amewahamasisha viongozi hao kwenda kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kupiga kura kuchagua viongozi bora.
" tukahamasishe wananchi, uchaguzi ufanyike kwa amani na tupate viongozi bora" amesema Msimamizi wa uchaguzi Dkt Mkoga
Katika kikao hicho ameshiriki Katibu Tawala wa Wilaya Ndugu Mohamed Ngasinda ambaye amewahamasisha wajumbe wa kikao hicho kwenda kutoa elimu ya mpiga kura kwa wananchi huku akiwasisitiza viongozi wa dini kutumia muda wa siku za ibada kuwahamasisha waumini kujitokeza siku ya uchaguzi.
Uchaguzi wa Serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024 ambapo Wenyeviti wa vijiji, wenyeviti wa vitongoji na wajumbe wa Serikali ya kijiji watachaguliwa.
Viongozi walioshiriki kikao hicho wameahidi kwenda kuhamasisha wananchi huku viongozi wa dini wakiwakaribisha Msimamizi wa uchaguzi na Katibu Tawala kutembelea nyumba za ibada ili kuwahamasisha waumini kushiriki uchaguzi.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.