Balozi wa zao la Pamba Tanzania Mhe. Agrey Mwanri akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija wametoa elimu kwa wakulima wa zao la pamba wa vijiji vya Manayi, Shigangama na Shilembo.
Elimu hiyo imetolewa leo Novemba 14,2024 katika mikutano iliyofanyika ikilenga kuwakumbusha wakulima kuzingatia sheria na taratibu za kilimo bora
" nitoe wito kwa wakulima wote kuwa kuanzia leo maotea yote yang'olewe shambani baada ya mwezi mmoja nitapita kukagua nitakayekuta hajayaondoa nitamchukulia hatua" amesema DC Ludugija
Akitoa elimu kwa Wananchi walioshiriki vikao hivyo Mwanri amesema ili kilimo kiwe na tija ni lazima kanuni bora zifuatwe ikiwa ni pamoja na kuandaa shamba la pamba kwa kuondoa maotea yote na kuyachoma, kupanda mbegu bora kwa kuzingatia kupanda kwa msitari na kwa vipimo vinavyoelekezwa, kupalilia kwa wakati na kunyunyizia viuwadudu kwa kufuata maelekezo.
Viongozi hao wamefika kwenye mashamba ya Pamba na kuwakuta baadhi ya wakulima wakiandaa mashamba yao hapo wameshirikiana nao kung'oa maotea na kuyachoma ikiwa ni mfano halisi wa namna ya kuteketeza maotea.
Wakulima walioshiriki mafunzo hayo wameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwajali wakulima wa zao la pamba kwani hivi karibuni wakulima hao walipewa baskeli kwaajili ya kuwarahisishia usafiri wa kufika shambani na kutembeleana ili kuhamasisha watu wengine kulima zao hilo.
Pia Serikali haijaishia hapo kwani wakulima wa zao la pamba wilayani Kwimba wamepewa trekta tano kwaajili ya kulima mashamba ya pamba.
Pamba ni zao la biashara linalolimwa na wakulima wengi wa Wilaya ya Kwimba, hivyo wananchi wameendelea kuhamasishwa kulima zao hilo ili waweze kujiongozea kipato na kukuza uchumi wa Familia na Taifa kwa ujumla.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.