Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba Ndugu Mohamed Ngasinda amekabidhi baskeli 60 kwa wakulima wa zao la pamba kutoka vijiji tofauti vya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
Vifaa hivyo vimetolewa leo Oktoba 31,2024 kwenye kituo cha polisi Ngudu zilipokuwa zimehifadhiwa " mnapewa baskeli hizi mkazitumie kwa lengo lililokusudiwa siyo kubebea mkaa, ila kuhakikisha mnakuwa wasaidizi wa maafisa ugani kwa kuwatembelea wakulima wenzenu wa pamba na kuwapatia ushauri pale inapohitajika" amesema Ngesinda
Baskeli hizo zimetolewa na Katibu Tawala kwa niaba ya bodi ya Pamba ambao wamelenga kuboresha kilimo cha pamba kwa kuwaandaa wakulima wachache kuwa mabalozi kwa wenzao kwa kuwafundisha kilimo bora na kuwatembelea marakwamara ili kubaini changamoto zinazoweza kujitokeza msimu wa kilimo.
Wakulima waliokabidhiwa vifaa hivyo wamepata mafunzo yatakayowawezesha kuwasaidia wakulima wengine kulima kilimo cha kisasa chenye tija.
" ninaishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia baskeli hizi maana zitaturahisishia kutembelea mashamba yetu na kuwatembelea wakulima wengine kuwafundisha kilimo bora "amesema Ngulimi Mkulima kutoka kijiji cha Kilyaboya
Serikali ya awamu ya sita imeendelea kuwaneemesha wakulima wa zao la pamba hapa Wilayani Kwimba kwani hivi karibuni wakulima hao walikabidhiwa trekta tano kama ruzuku kwaajili ya kuwarahisishia kilimo cha zao hilo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.