• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

Wakuu wa Mikoa nane wa Kanda ya Magharibi Wafanya Ziara ya Mafunzo ya Kilimo cha Pamba Wilayani Kwimba

Posted on: May 15th, 2017

Wakuu wa Mikoa nane  inayojishughulisha na kilimo cha Pamba   ambayo ni  Geita, Kagera, Kigoma, Singida, Simiyu, Shinyanga, Tabora na Mwanza  wamefanya ziara   Wilayani  Kwimba  kwa ajili ya kujifunza mbinu mbalimbali za kufufua zao la pamba ambalo kwa takribani miaka mitano uzalishaji wake umeshuka.

Akisoma taarifa kwa Wakuu wa Mikoa hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba  Mhe. Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon  alisema  Wilaya ya Kwimba imenufaika kupitia  kilimo cha pamba cha mkataba kwa kuwapatiwa pembejeo za mkopo, uwezeshwaji wa huduma za ugani kutoka kwa makampuni na  uundaji wa vikundi vya wakulima (FBGs).

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya alisema kilimo cha Pamba kinachangamoto ya Upungufu wa mvua uliosababisha wakulima wengi kushindwa kupanda mbegu za pamba na wengine ambao walikuwa wameshapanda kurudia tena kutokana na mbegu walizopanda mara ya kwanza kutoota kabisa.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John .V.K.Mongella, alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Mhandisi Mtemi Msafiri Simeoni  kwa kusimia vizuri mikakati iliyotumika kufanikisha Kilimo cha Mkataba Wilayani Kwimba wakati ya ziara ya utembelea shamba la pamba la Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama(W) na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba. Aliendelea kusema kuwa, Wilaya ya kwimba ndiyo Wilaya kinara kwa Mkoa wa Mwanza kwa kulima pamba, hivyo amempongeza sana Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon  kwa  mchango wake wa hali na mali wa kufanikisha kilimo cha pamba  Wilayani Kwimba.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa singida Dkt.Rehema Nchimbi aliongezea kwa kumuomba Mkuu wa wilaya ya Kwimba awapatie  vibarua wanaovuna  pamba vifaa vya kuzuia vumbi  ili kuepukana na vumbi kuingia kwenye  njia ya hewa kwani bila kufanya hivyo vibarua hao afya zao zitakuwa hatarini.

Naye Ndg Bulugu Furano ambaye ni mkulima wa  zao la pamba katika kijiji cha Isunga alisema pamba yake  imeshambuliwa na wadudu  aina ya ‘thrips’ na kusababisha  pamba kunyauka na kudondosha majani na vitumba ambavyo havijakomaa, hivyo ameiomba Serikali kuhakikisha inapiga marufuku usambazaji wa dawa bandia kwa wakulima. Mkulima mwingine Ndg Buruma Nzobe aliongezea kwa kuiomba Serikali kupanga na kutangaza bei itakayomnufaisha mkulima kwani mpaka sasa bado Serikali haijatangaza rasmi bei ya pamba itakayotumika katika msimu huu.

Akitoa maelezo ya kuhitimisha  ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri amewaomba wakulima wa pamba wazalishe pamba safi na amesisitiza kuwa hakuna mtu atakaeuza wala kununua Pamba chafu.

Tokea miaka ya 1980 Wilaya ya Kwimba ilikuwa miongoni mwa Wilaya za kuigwa katika kanda ya ziwa kwa uzalishaji wa zao la pamba ikufuatiwa na Wilaya ya Maswa.

 

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.