Ibada maalumu ya kuombea Taifa la Tanzania kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika 29, Oktoba 2025 imefanyika leo katika shule ya Sekondari Ngudu ambapo wanafunzi wakiongozwa na Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Wilbard Mchele wamemuomba Mungu aendeleze amani, umoja na mshikamano
" sisi kama Taifa tunatakiwa tuombe Mungu atusimamie na kutupatia amani katika kipindi hiki cha uchaguzi na baada ya uchaguzi, kwahiyo tuombe na tunaamini uchaguzi utafanyika salama" amesema Mchele
Aidha Mkuu huyo amewataka wanafunzi wote kwenda kuwa mabalozi kwa kuwahamasisha wazazi wao na walezi wao kwenda kupiga kura siku ya uchaguzi ili kuweza kupata viongozi bora watakaoleta maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Ibada hiyo imeongozwa na mwinjilist Mhandisi Alistides Leopord ambaye amewaasa wanafunzi hao kuwa na tabia nzuri " elimu bila tabia njema siyo kitu, mnatakiwa kumpenda Mungu ili awapatie hekima ya kuchagua kutenda matendo mema" amesema
Mhandisi Leopord amesisitiza kuwa vijana hao wanapaswa kuongozwa na Mungu katika kufanya maamuzi hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu.
Wanafunzi walioshiriki ibada hiyo wameeleza jinsi walivyojiandikisha na wako tayari kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka
" ibada ya leo imetuunganisha madhehebu yote na tumemuomba Mungua aendeleze amani ya Taifa letu,pia sisi tuko tayari kwenda kupiga kura ifikapo Oktoba 29,2025 na tunawashauri vijana wenzetu kwenda kupiga kura ili tupate viongozi tunaowataka" amesema Michael



Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.