• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

WANANCHI WA KADASHI WAAHIDI KUJITOLEA NGUVU NA MALI KUFANIKISHA UJENZI WA SHULE MPYA

Posted on: July 25th, 2022

Wananchi wa kijiji cha Kadashi Kata ya Maligisu wameahidi kujitolea mali na nguvu ili kufanikisha uanzishwaji wa  ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi.


Ahadi hizi zimetolewa leo tarehe 25,Julai 2022 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika  kati ya Wananchi na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe Johari Samizi, mkutano uliolenga kuwahamasisha Wananchi kujitokeza kushiriki ujenzi wa madarasa unaotarajiwa kuzinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  tarehe 1,Agosti 2022.


Akiongea katika mkutano huo Mkuu wa Wilaya amewaeleza Wananchi kuwa Serikali inaendelea kutekeleza miradi mingi katika kijiji hicho ikiwemo ujenzi wa Kituo cha Afya uliofikia hatua za ukamilishaji na miradi mingine, amesisitiza kuwa ujenzi wa madarasa utasaidia wananfunzi wa Shule ya  msingi kusoma katika mazingira mazuri bila msongamano darasani.


Aidha Mheshimiwa Samizi ameutumia mkutano huo kuwataka Wananchi kuhifadhi chakula ili kujiepusha na hatari ya njaa inayoweza kujitokeza.

" tunakoelekea tunakwenda kwenye njaa ya ajabu kwa sababu mmevuna chakula kingi lakini mnakiuza chote, nawaeleke kila familia kuhakikisha mnatunza chakula cha akiba msiuze mazao yote, mtapata njaa na hakuna chakula cha msaada" amesema Samizi


Mheshimiwa Samizi ameutumia mkutano huo kutoa elimu ya umuhimu wa sensa, amewataka wananchi waliohudhulia mkutano huo kuwa mabalozi kwa watu wengine kuhamasisha watu wote kujitokeza kuhesabiwa tarehe 23, Agosti 2022. Amesema kuwa kupatikana kwa idadi kamili ya Wananchi waliopo katika kila eneo kutarahisishia Serikali kutoa huduma sahihi kwa watu sahihi.


" Serikali ikiwa na takwimu sahihi za idadi ya watu wanaoishi  kila eneo mfano Kadashi italeta wahudumu wa Afya kulingana na wingi wa watu, itatengeneza miundombinu na vitu vingine kulingana na uhitaji, hivyo niwaombe mjitokeze kuhesabiwa na msiwafiche walemavu nao wanahaki ya kuhesabiwa" amesema Samizi

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.