Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija amewahamasisha Wananchi kujitokeza kupiga kura siku ya uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024.
Hamasa hiyo imefanyika leo tarehe 23,Novemba ,2024 kwenye viwanja vya Kwideco ambapo bonanza la michezo mbalimbali limefanyika.
" wananchi wote tujitokeze kupiga kura siku ya uchaguzi ili tukawachague viongozi tunaowataka ambao watahamasisha maendeleo katika maeneo yetu" amesema Ludigija
Naye msimamizi wa Uchaguzi Dkt Amon Mkoga ametumia wasaa huo kuwahamasisha wananchi wote waliojiandikisha wajitokeze kupiga kura
Amesisitiza kuwa elimu ya mpiga kura imetolewa kwa wananchi kupitia njia mbalimbali ikiwemo, vyombo vya habari, mikutano, mitandao ya kijamii, vipeperushi na matangazo.
" tunawahamasisha kila mwananchi aliyejiandikisha awe tayari kwenda kupiga kura, elimu imetolewa hivyo tunaamini wananchi watapiga kura" amesema Mkoga
Wananchi walioshiriki bonanza hilo wameeleza utayari wao wa kushiriki uchaguzi huo " lazima nikapige kura siku hiyo maana natamani kiongozi ninaye mtaka ndio awe mshindi" amesema Justina Nyanda
Katika bonanza hilo hamasa imetolewa kupitia mchezo wa mpira wa miguu ambapo timu iliyoibuka mshindi ( Bodaboda FC ) imejinyakulia Mbuzi na timu iliyoshika nafasi ya pili ( Modo FC ) imepata mbuzi, na washindi wa michezo mingine wamepata zawadi mbalimbali.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.