Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija amehamasisha Wananchi kushiriki uchaguzi kwa kuhakikisha kila mtu anatimiza haki yake ya kupiga kura
"Nitumie nafasi hii kuwaalika wananchi wote wa majimbo haya kuwa uchaguzi ni vema kushiriki kupiga kura ili tuchague viongozi sahihi,tutumie muda huu uliobaki kuhudhuria kampeni na kusikiluza sera ili tukachague viongozi sahihi" amesema Ludigija
Mheshimiwa Ludigija amewahakikishia wananchi kuwa siku ya uchaguzi kutakuwa na usalama wa kutosha hivyo wananchi wote wajitokeze kupiga kura kuchagua viongozi watakaohamasisha maendeleo ya Taifa.
Pia amewataka wachezaji wote walioshiriki bonanza hilo kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanacheza michezo yote vizur bila kusababishiana majeraha yanayoweza kuwasababishia kushindwa kufanya kazi nyingine au kushiriki uchaguzi
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Dkt.Amon Mkoga ametumia wasaa huo kuwahimiza wananchi wote kuendelea kuhamasishana ili wananchi wote wajitokeze kupiga kura ili kutimiza haki yao yamsingi
" niwahamasishe kila mtu siku ya uchaguzi ampitie ndugu yake au rafiki yake kwenda kupiga kura, tuhamasishane wote tushiriki kuwachagua viongozi wetu" amesema Mkoga
Katika bonanza hilo wameshiriki wananchi wa Kwimba na wanamichezo kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Manispaa ya Ilemela, Halmashauri ya Magu,Misungwi,Halmashauri ya Ukerewe,Halmashauri ya Buchosa na mwenyeji Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.



Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.